Rais wa Jamhuri ya Angola, Mhe. João Manuel Gonçalves Lourenço, amehitimisha ziara yake ya kitaifa ya siku tatu nchini na kuondoka kurejea nchini Angola, Oktoba 30, 2026.
Katika ziara hiyo, Rais Lourenço alifanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhusu masuala mbalimbali ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kupanua ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo kati ya mataifa hayo mawili.
Akiwa jijini Dodoma, Rais Lourenço alishiriki hafla ya uzinduzi wa Mji wa Serikali Mtumba pamoja na miundombinu ya barabara zake.
Mheshimiwa Lourenço aliagwa rasmi na mwenyeji wake Rais Samia katika Viwanja vya Ikulu Chamwino Dodoma kabla ya kuelekea Uwanja wa Ndege wa Dodoma.
Katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma Mheshimiwa Lourenço alisindikizwa na kuagwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb.) Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Balozi wa Tanzania anayewakilisha Angola mwenye makazi yake Zambia Injinia Cyprian Luhemeja, Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Angola Bw. Mbwana Mziray na viongozi wengine wa Serikali.















Post A Comment: