Kizimkazi, Kusini Unguja — Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Prof. Hamisi Masanja Malebo, ameungana na viongozi wengine wa Wizara katika kumtembelea na kumpa pole Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mume wake, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.

Ziara hiyo imefanyika tarehe 11 Septemba 2026 nyumbani kwa Rais Samia, Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, ambapo ujumbe huo ulifika kutoa pole na faraja kwa Rais pamoja na familia yake katika kipindi hiki cha maombolezo.

Prof. Malebo, akiwa sehemu ya ujumbe huo wa viongozi, aliungana na viongozi wengine wa Wizara kuwasilisha salamu za pole kwa Rais Samia na familia yake kufuatia msiba wa Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan, aliyefariki dunia tarehe 7 Septemba 2026 katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena, Zanzibar.



Tume ya Taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaungana na Rais Samia, familia, ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huo katika kipindi hiki cha huzuni na maombolezo.

Tume inatoa pole kwa Rais Samia na familia yake, huku ikiwaombea nguvu, faraja na moyo wa subira katika kipindi hiki cha majonzi.

Tume ya Taifa ya UNESCO inaendelea kuungana na familia katika kuomboleza msiba huo na kuenzi kumbukumbu ya Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.


Share To:

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: