Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere leo imewaaga rasmi wajumbe wawili wa bodi ya Chuo hicho ambao wamemaliza muda wao tangu walipoteuliwa kushika nafasi hizo kwa kipindi cha miaka mitatu.
Wajumbe walioagwa ni pamoja na Prof. David Mfinanga na Ally Kibona ambao waliteuliwa Agosti 2023 na kuwa hadi Agosti 2026 wanatimiza miaka mitatu ya kutumikia nafasi hizo.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wajumbe hao, Mwenyekiri wa bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mhe. Stephen Wasira amewashukuru Wajumbe hao waliomaliza muda wao kwa utumishi wao na mchango walioutoa katika kuhakikisha masuala mbalimbali yanayohusu taasisi yanakwenda sawa.
Mhe. Wasira amesema Chuo kinathamini na kutambua michango yao waliyokuwa wanaitoa wakati wa kutimiza majukumu yao kupitia vikao na ziara mbalimbali za kikazi ambazo wamekuwa wakizifanya.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo amewapongeza na kuwashukuru kwa kipindi cha miaka mitatu kwa kutumikia nafasi zao kwa uaminifu, uadilifu na ushirikiano waliounesha kwa wajumbe wengine wa bodi hiyo kwa lengo la kuhakikisha Chuo kinatimiza malengo yake.
Nao Wajumbe waliomaliza muda wao ambao ni Prof. David Mfingana na Ally Kibona wamewashukuru wajumbe waliobakia kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiupata kutoka kwenye bodi hiyo kwa muda wote waliokuwa wakitumikia nafasi zao, vilevile wamejifunza mengi kutoka kwa viongozi ambao walikuwa wakifanya nao kazi.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasilano na Masoko
CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
7.08.2026

Post A Comment: