Mfanyabiashara maarufu nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa Group, Rostam Azizi, akizungumza katika Jukwaa la Nne la Biashara la Watendaji Wakuu 200 (200 CEOs Business Forum).
Mfanyabiashara maarufu nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa Group, Rostam Azizi, akizungumza katika Jukwaa la Nne la Biashara la Watendaji Wakuu 200 (200 CEOs Business Forum)
Mfanyabiashara maarufu nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa Group, Rostam Azizi, akiwa katika Jukwaa la Nne la Biashara la Watendaji Wakuu 200 (200 CEOs Business Forum)
***
Mfanyabiashara maarufu nchini na kanda ya Afrika na Mwenyekiti wa Taifa Group , Rostam Azizi, amehimiza uwepo wa uongozi imara, taasisi madhubuti, sera nzuri na uwazi wa mifumo ili kufungua zaidi fursa za uwekezaji na mitaji ya kimataifa katika nchi za kanda ya Afrika Mashariki.
Akiongea kwenye Jukwaa la nne la Biashara la Watendaji wakuu 200 (200 CEOs Business Forum) linalowakutanisha pamoja wafanyabiashara na wawekezaji nchini, alisema ushirikiano wa kweli kati ya wawekezaji, wafanyabiashara na Serikali utajengwa kwenye misingi ya mifumo mathubuti ya kikodi, kisera kikanuni na sheria nchini na kwenye nchi nyinginezo za Afrika Mashariki.
Rostam alisema wadau wote wanapaswa kujikita kuangalia ni kwa namna ipi tunaweza kuifanya Afrika Mashariki kuwa chaguo kuu la uwekezaji wa mitaji ya mitajiya kimataifa.
“Nianze kwa kuwapongeza waandaaji wa Kongamano la Biashara la Wakurugenzi Wakuu 200 (200 CEOs Business Forum) kwa kuwaleta pamoja viongozi wa Serikali, Sekta binafsi na wawekezaji na suala la msingi la kujadili ni jinsi gani tuanaweza kuifanya Afrika Mashariki kuwa chaguo kuu la mitaji wa kimataifa”, alisema Rostam Azizi.
Alisema rasilimali nyingi za asili, idadi ya watu na eneo la kijiografia havitoshi kuhakikisha uwekezaji wa muda mrefu kutoka kwa wawekezaji wa kimataifa kuja kuwekeza bali pia kunatakiwa uwepo mazingira ya kuwakikishia uhakika,utulivu ,ukuaji na kuwajengea imani.
Alisisitiza jukwaa hili kutoka na maamuzi yenye kuleta athari kubwa kwa utekelezaji wa mitaji na pamoja na mambo mengine kujua sekta zinazokua na ajira jinsi ya utengenezaji wa ajira mpya ndani ya Afrika Mashariki sambamba na kujua taasisi za kifedha zinazowezesha biashara na ufadhili, viwanda vinavyoongeza thamani ya fedha, makampuni ya madini yanayofungua fursa za rasilimali na makampuni ya mawasiliano yanayofanya vizuri ili kuwaunganisha mamilioni ya watu ndani ya Ukanda wa Afrika Mashariki.
“Niruhusuni kuzungumza kutokana na uzoefu wangu, katika kipindi cha zaidi ya miaka thelathini, kupitia Taifa Group pamoja na washirika wetu mbalimbali, nimepata fursa ya kuwekeza katika sekta za mawasiliano, madini, nishati, usafiri wa anga, vyombo vya habari na miundombinu,” amesema Rostam Azizi.
Aliongeza kwamba watu wengi hudhani kuwa uwekezaji unaanza na uchambuzi wa kifedha ambapo si kweli bali wawekezaji wengi wanataka imani na mwelekeo wa nchini husika pamoja na makubaliano kuheshimiwa na sera ambazo zinaweza kutabirika.
Pamoja na mambo mengine alilisitiza umuhimu wa kuwa na taasisi imara na zenye kuaminika na kanuni zilizo wazi na mazingira mazuri ya uwekezaji na madhubuti yanayoweza kutabirika kisheria na kitaasisi ambayo yataleta matokeo chanya.
Alisema Afrika Mashariki si eneo la matarajio pekee ni fursa halisi ambayo inahitaji mageuzi ya haraka ya kidigitali, na mikakati kabambe ya kufikia njia kuu za biashara za dunia ili kufugua milango ya fursa ya mitaji ya kimataifa.
“Ari ya ujasiriamali ndani ya Afrika mashariki na ukauaji wa soko la walaji ni fursa ya kipekee wa wanajumuiya wa kuunganisha nguvu pamoja ili kuleta mapinduzi ya kweli kwenye uwekezaji. Tanzania iko katikati ya fursa hiyo na bandari zetu zinaunganisha uchumi wetu pamoja na nchi jirani zisizo na bandari na dunia tambayo hutoa fursa ya kufikia masoko ya kikanda na kimataifa,”alisisitiza.
Aliongeza kwamba uwekezaji katika bandari, reli ya Standard Gauge Railway (SGR) , nishati , mifumo ya usafirishaji na mawasiliano ya kidigitali unaimarisha nafasi hiyo kwa kupunguza gharama za biashara na kuongeza tija.
Alisema kwa pamoja , nchi za Afrika Mashariki zinawakilisha soko la zaidi ya watu milioni 300, ikiwa na rasilimali nyingi za asili , idadi kubwa ya vijana na miundombinu inayozidi kuimarika.
“Hakuna nchi moja katika ukanda wetu yenye kila faida ya ushindani , hakuna uchumi mmoja wenye kila rasilimali, hakuna soko moja linaloweza kufikia uwezo wake kamili likiwa peke yake,” alisisitiza.
Rostam Azizi alisema ni muhimu kwa serikali za Afrika Mashariki kuanza mchakato wa kuimarisha miumdombinu inayovuka mipaka , kupunguza vikwazo vya kibiashara , kuimarisha ushirikiano wa kifedha na kurahisisha usafirishaji wa mitaji, bidhaa na wataalamu wenye ujuzi ndani ya ukanda huo.
Aliongeza kuwa jukumu la serikali, ni kuendelea kujenga mazingira bora na yanayotabirika kwa uwekezaji na biashara na inajumuisha kudumisha uthabiti wa uchumi wa jumla, kuimarisha miundombinu, kuboresha mazingira ya udhibiti, kuwezesha uwekezaji, kuongeza upatikanaji wa mitaji na kuimarisha taasisi za umma.
Alitoa rai kwa sekta binafsi kuhakikisha zinaongeza tija huku zikiimarisha utawala bora katika biashara zao na kutumia teknolojia za kisasa pia ziendeleze rasilimali watu na zijenge biashara zinazoweza kushindana ndani ya Tanzania, Afrika Mashariki na kwingineko.












Post A Comment: