Meneja wa EWURA Kanda ya Magaharibi, Mha. Karim Ally(kushoto) akitoa maelezo ya majukumu yanayotekelezwa na Mamlaka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Mh. Dkt. Rashid Chuachua(kulia) ikiwemo utoaji wa leseni na vibali vya ujenzi wa vituo vya mafuta, vituo vya CNG, utatuzi wa migogoro na malalamiko na nafasi ya EWURA katika kuweka mazingira wezeshi ya kupata wasambazaji wakubwa wa gesi ya mitungi ( LPG) katika eneo la Kanda ya Magharibi linalohudumia mikoa ya Tabora, Shinyanga, Katavi na Kigoma, wakati kuongozi huyo alipotembelea banda la EWURA katika maonesho ya NaneNane yanayoendelea viwanja vya Ipuli, Tabora, leo 02/08/2026.
Na.Mwandishi Wetu-Tabora
Wakuu wa Wilaya za Tabora, Mh. Upendo Wella, na Kigoma, Mh. Dkt. Rashid Chuachua, wameipongeza EWURA kwa usimamizi mzuri wa huduma za nishati na maji nchini. Wametoa pongezi hizo walipotembelea banda la EWURA, katika maonesho ya NaneNane yanayoendelea viwanja vya Ipuli, Tabora, leo, 02.08.2026.
Viongozi hao wameitaka EWURA kuongeza hamasa kwa wananchi ili kubadili mtazamo na kuhamia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia ili azma ya kufikia 80% ya watumiaji ifikapo 2034 itimie.
Aidha, wameisisitiza EWURA kuendelea kuhamasisha uwekezaji wa vituo vya mafuta maeneo ya vijijini, wakieleza kuwa huduma hiyo inahitajika kutokana na kushamiri shughuli za kilimo, ufugaji na uvuvi.
Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Mha. Karim Ally, alitumia fursa hiyo kueleza nafasi ya EWURA ya kuweka mazingira wezeshi ya kupata wasambazaji wakubwa wa gesi ya mitungi (LPG) katika eneo la Kanda ya Magharibi linalohudumia mikoa ya Tabora, Shinyanga, Katavi na Kigoma, ambapo kwa sasa ni 19 pekee.

Meneja wa EWURA Kanda ya Magaharibi, Mha. Karim Ally(kushoto) akitoa maelezo ya majukumu yanayotekelezwa na Mamlaka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Mh. Dkt. Rashid Chuachua(kulia) ikiwemo utoaji wa leseni na vibali vya ujenzi wa vituo vya mafuta, vituo vya CNG, utatuzi wa migogoro na malalamiko na nafasi ya EWURA katika kuweka mazingira wezeshi ya kupata wasambazaji wakubwa wa gesi ya mitungi ( LPG) katika eneo la Kanda ya Magharibi linalohudumia mikoa ya Tabora, Shinyanga, Katavi na Kigoma, wakati kuongozi huyo alipotembelea banda la EWURA katika maonesho ya NaneNane yanayoendelea viwanja vya Ipuli, Tabora, leo 02/08/2026.

Meneja wa EWURA Kanda ya Magahribi, Mha. Karim Ally(kulia) akimweleza Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Mh. Upendo Wella (kushoto), Mamlaka inavyoendelea kutoa elimu na kuhamasisha ujenzi wa vituo maeneo ya vijijini ambapo uhitaji bado ni mkubwa hususan katika maeneo ya pembezoni na hivyo kuendelea kuwepo uuzaji holela wa bidhaa za petroli, ambao ni hatari kwa afya, mazingira na maisha ya watu, wakati kiongozi huyo alipotembelea banda la EWURA, katika maonesho ya NaneNane, viwanja vya Ipuli, Tabora, leo, 02/08/2026.

Post A Comment: