Kukamilika kwa ujenzi wa Daraja la Upinde la Mawe katika Mto Mmbaga, Wilaya ya Ngorongoro, kunatarajiwa kufungua fursa za kijamii na  kiuchumi kwa kurahisisha usafiri na usafirishaji, kuboresha upatikanaji wa huduma za kijamii pamoja na kuchochea biashara kwa wakazi wa eneo hilo na maeneo jirani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa daraja hilo katika mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2026, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Michael Mwang'onda, amesema kuwa mradi huo umeondoa adha ya muda mrefu iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa maeneo hayo, hususan kipindi cha msimu wa mvua ambapo ilikuwa changamoto kubwa kuvuka Mto Mmbaga. 

Amesisitiza kuwa, Serikali ya awamu ya sita imeendelea kuboresha miundombinu ya barabara kwa kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika ujenzi wa barabara na madaraja ili kuimarisha miundombinu na kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.

"Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alitambua changamoto zilizokuwa zinawakabili wananchi wa eneo Oldonyosambu na majirani zake na kuelekeza fedha zitolewe kwa ajili ya ujenzi wa daraja hili, ambalo sasa limekuwa mkombozi kwa jamii, tuendelee kulitunza na kulitulitumia kwa usafirishaji wa watu na bidhaa, kupanua fursa za biashara na kuimarisha shughuli za kiuchumi kwa maendeleo yetu na Taifa letu," Amesema Mwang'onda.

Mwang'onda amesisitiza kuwa, Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini huku akiwahimiza wananchi kuendelea kudumisha amani na utulivu, ambayo ni msingi wa maendeleo endelevu.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro, Yanick Ndoinyo, alipokea kwa furaha kukamilika kwa daraja hilo akisema linahudumia kata za Sale, Pinyinyi na Oldonyosambu kupitia Masusu hadi Jema

Alimshukuru Rais Dk,Samia Suluhu Hassan kwa kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi wa Ngorongoro kwa kutoa fedha za Mfuko wa Barabara  zilizowezesha ujenzi wa daraja hilo, akieleza kuwa ni hatua muhimu katika kuboresha mawasiliano, usafiri na maisha ya wananchi wa wilaya hiyo.









Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: