Siku zote alikuwa miongoni mwa wale wanaopinga imani yoyote inayohusiana na mambo ya kiroho au usaidizi wa kipekee nje ya hospitali na sheria za kawaida.

Jina lake ni Brian, na alikuwa rafiki yangu wa karibu tangu chuo kikuu. Mcheshi, mwenye akili nyingi, lakini mwenye misimamo mikali isiyoyumba hasa linapokuja suala la imani zisizo za kisayansi.

Lakini maisha ni walimu wakubwa kuliko vitabu. Na wakati mwingine, hata wasioamini, hupata sababu ya kufikiri upya. Brian alikuwa kwenye uhusiano wa muda mrefu na msichana aitwaye Hellen. Walikuwa kama mfano wa wapenzi bora mitandaoni. Picha za mapenzi, safari, zawadi ilikuwa ni hadithi ya kisasa ya upendo.

Hata hivyo, mambo yalianza kubadilika mwaka jana, pale Brian alipogundua kwamba Hellen alikuwa akiongea kwa karibu sana na jamaa mmoja wa kazini kwake. Awali alipuuzia, akiamini ni wivu tu wa kawaida. Lakini alipoanza kuona ujumbe mfupi wa siri, mazungumzo ya sauti usiku wa manane, na safari za ghafla zisizoelezeka, alijua kuna jambo. SOMA ZAIDI.
Share To:

Post A Comment: