Nilijua wazi kuwa ardhi ile ilikuwa yangu kihalali. Niliinunua kwa jasho langu mwenyewe baada ya miaka mingi ya kufanya kazi ndogo ndogo, kujiwekea akiba, na hatimaye kupata kipande hicho cha ardhi kando ya mto katika kijiji cha baba yangu. Ilikuwa sehemu niliyoipenda sana, na ndoto yangu ilikuwa ni kujenga nyumba ndogo ya kupumzikia baada ya kustaafu kazi ya ualimu.

Lakini mambo yalibadilika nilipopata taarifa kwamba kijana mmoja wa ukoo, ambaye sikuwa hata na ukaribu naye, alikuwa ameweka uzio na kuanza kulima kwenye ardhi yangu kana kwamba ni yake. Nilipokwenda kumhoji, alinikaripia na kusema kuwa hiyo ardhi ni ya familia, na mimi sina haki nayo kwa sababu sikuishi kijijini kwa muda mrefu.

Nilichanganyikiwa, nikamuonyesha stakabadhi za umiliki halali lakini bado alikataa kuondoka.
Nilifikisha suala hilo kwa uongozi wa kijiji, lakini hata hapo hakukuwa na msaada wowote wa maana. Kila mtu alionekana kumwogopa au kumfurahia kwa sababu ya pesa zake. Nikaamua kufungua kesi mahakamani, nikiwa na imani kwamba haki itatendeka.

Lakini niligundua kuwa hata kwenye mchakato wa kisheria, si kila kitu ni haki na uwazi. Mtu huyo alianza kutumia mbinu chafu, akijaribu kushawishi mashahidi wangu na hata kutoa rushwa kwa baadhi ya maafisa.SOMA ZAIDI.
Share To:

Post A Comment: