Kulikuwa na kipindi maishani mwangu ambapo niliamini kwamba maisha yangu yalikuwa yamepangwa tayari. Nilikuwa kwenye uhusiano wa miaka kadhaa na mtu ambaye nilimpenda kwa moyo wangu wote.

Tulikuwa tumezungumza kuhusu ndoa, maisha ya baadaye, na hata majina ya watoto tuliotamani kuwa nao siku moja. Nilikuwa na uhakika kwamba ndiye mtu ningeishi naye maisha yangu yote. Lakini siku moja kila kitu kilibadilika.

Bila kutarajia, alianza kuwa mbali. Mawasiliano yakapungua, mipango ikaanza kusogezwa mbele, na hali ambayo zamani ilikuwa ya furaha ikaanza kujawa na sintofahamu.

Kisha nikapokea maneno ambayo sikuwahi kutarajia kuyasikia. Aliniambia hataki kuendelea na uhusiano wetu. Kwa kweli nilivunjika moyo. Kilichoniumiza zaidi ni kwamba nilikuwa tayari nimejenga maisha yangu ya baadaye nikimhusisha yeye.

Ghafla ndoto zote nilizokuwa nimejenga zilionekana kuporomoka mbele ya macho yangu. Kulikuwa na usiku nilikosa usingizi. 

Nilikuwa nikijiuliza ni wapi nilikosea na kwa nini jambo lile limenitokea. Wakati mwingine nilihisi kama nisingeweza kumpenda mtu mwingine tena. SOMA ZAIDI.


Share To:

Post A Comment: