Siku ambayo nilipokea taarifa kwamba harusi yetu haitafanyika ndiyo siku niliyohisi moyo wangu ukivunjika zaidi kuliko wakati mwingine wowote maishani mwangu.

Mimi na mpenzi wangu tulikuwa tumepanga harusi kwa miezi mingi. Familia zote mbili zilikuwa zimejiandaa, wageni walikuwa wamealikwa, na mipango mingi ilikuwa imekamilika. Nilikuwa nikihesabu siku zilizobaki kabla ya kuanza maisha mapya ya ndoa.

Lakini wiki mbili kabla ya harusi, kila kitu kilibadilika. Mpenzi wangu aliniambia kuwa alihitaji kusitisha harusi. Nilihisi kama dunia ilisimama kwa sekunde chache. 

Sikuelewa kilichokuwa kinaendelea. Nilijaribu kuuliza maswali mengi, lakini majibu hayakuwa wazi vya kutosha kunipa amani.

Kwa kweli iliniumiza sana. Kilichoniumiza zaidi ni kuwaeleza ndugu, marafiki, na watu waliokuwa tayari wamepanga kuhudhuria harusi. Nilihisi aibu, huzuni, na kuchanganyikiwa kwa wakati mmoja. SOMA ZAIDI.
Share To:

Post A Comment: