Nilipoanzisha biashara yangu, nilikuwa na matumaini makubwa sana. Nilikuwa naamini kwamba bidhaa zangu zingepata soko haraka na maisha yangu yangeanza kubadilika. 

Nilitumia akiba yangu kununua bidhaa, nikafungua ukurasa wa Facebook, na kuanza kutangaza kila siku.

Lakini mambo hayakwenda kama nilivyotarajia. Kila nilipopost bidhaa zangu, watu walikuwa wanapenda picha na wakati mwingine kuacha comments, lakini hakuna aliyekuwa akinunua. Siku zikageuka wiki, wiki zikageuka miezi, na bado mauzo yalikuwa karibu sifuri.

Kwa kweli nilivunjika moyo. Kilichoniumiza zaidi ni kuona biashara nyingine zikikua kupitia Facebook huku mimi nikihangaika kupata hata mteja mmoja wa kweli. Wakati mwingine nilikuwa natumia pesa kutangaza posts lakini matokeo yalikuwa madogo sana.

Nilianza kujiuliza kama nilifanya makosa kuanzisha bibiashara. Kulikuwa na siku nilifikiria kuacha kabisa na kuuza bidhaa nilizokuwa nimebaki nazo. SOMA ZAIDI.
Share To:

Post A Comment: