NAIBU Waziri wa Madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Longido Mkoani Arusha, Dkt Steven Kiruswa amewataka wananchi wa jimbo hilo kujenga umoja na wananchi wa nchi jirani ya Kenya kwani viongozi wa juu ya nchi hizo wanamahusiano mazuri na hivyo nao wanapaswa kufuata nyayo hizo.
Kiruswa alisema hayo juzi katika kijiji cha Kimwat kilichopo kata ya Sinonik wilayani Longido ambacho kipo mpakani mwa Kenya wakati akizindua miradi miwili ya maendeleo ikiwemo mradi wa Zahanati na mradi wa maji vyote vikiwa na gharama ya zaidi ya shilingi milioni 188.3 miradi hiyo imetekelezwa kwa mchango wa Mbunge Kiruswa , nguvu za wananchi,shirika lisilo la kiserikali la Pingo's na fedha kutoka serikali kuu.
Alisema kijiji hicho na kata kwa ujumla walikuwa wakipata huduma ya maji ,elimu na afya katika nchi jirani ya Kenya kutokana na mahusiano mazuri waliyajenga na wananchi wa nchi hizo lakini awamu ya sita ya uongozi wa serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan huduma hiyo inapatikana nchini na sasa wananchi wa Kenya wanakuja kupata huduma hizo hapa nchini.
Kiruswa alisema kutokana na uhusiano mzuri na wananchi wa Kenya na Tanzania ndio màana Uzinduzi wa miradi hiyo umehudhuriwa wananchi wa nchini humo wakiongozwa na viongozi wao akiwemo Afisa Mtendaji Kijiji cha Meto,Peter Milia na Joseph Kink Afisa Mtendaji wa Kata ya Meto.
Alisema mradi wa Zahanati ulianza kujengwa june 2023 na kukamilika mwaka huu yeye binafsi amechangia kiasi cha shilingi milioni 5,michango ya wananchi sh milioni 11 na fedha toka serikali kuu zilipelekwa shilingi milioni 80 na sasa Zahanati hiyo inahudumia wananchi wa Kijiji cha Kimwat na wananchi wa nchi jirani.
Naibu Waziri kiruswa aliipongeza Pingo’s kwa kusimamia na kutoa fedha shilingi milioni 70 ,michango ya wananchi shilingi milioni 2.3 na Mbunge shilingi milioni 20 na kusema kuwa mradi huo utasaidia wananchi na wananchi na mifugo na utekelezaji huo ni kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) kufikisha huduma karibu na wananchi.
Naye Mkuu wa wilaya ya Longido ,Salumu Kally amewaomba wananchi wa Longido kumpa ushirikiano Mbunge Kiruswa kwani kiongozi mwenye upendo na wananchi wake na amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha huduma zote muhimu ikiwemo miradi ya Maji ,Afya ,elimu ,umeme na Barabara inakamilika kwa maslahi ya wananchi wake hivyo hapasŵi kupotezwa katika uongozi wake.
Naye Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kimwat Rosemary Mbogho wakati akisoma risala kwa mgeni rasmi Kiruswa alisema kijiji kinakabiliwa na changamoto ikiwemo upungufu wa watumishi wa Zahanati,nyumba za watumishi ,madarasa ,barabara na umeme katika vitongoji na Mbunge Kiruswa aliahidi yeye na marafiki zake kujenga nyumba ya watumishi na suala la barabara alimwagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini(TARURA) kutekeleza hilo kwani bajeti fedha hizo zipo.























































Post A Comment: