Viongozi mbalimbali wa Chama cha mapinduzi Mkoa na Wilayani wakiambatana na Viongozi wa Serikali mkoa wa Dodoma wameanza safari ya Kikazi kuelekea mkoani Mtwara kwenye Vyama Vikuu na Vyama vya Ushirika vya Msingi.

Viongozi hao wakingozana na Mrajis Msaidizi wa mkoa wa Dodoma Ndg Joseph Chitinka na Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoa wa Dodoma Bibi Theresia Nyoka wameanza ziara hiyo leo Mei 12, 2026 kutokea mkoani Dodoma kuelekea mkoani humo.

Mrajis Msaidizi wa mkoa wa Dodoma ameeleza lengo la ziara hiyo ni kuwajengea uwezo, kujifunza utekelezaji wa Mfumo wa stakabadhi za ghala na kujionea utekelezaji wa miradi mbalimbali kwenye Vyama Vikuu na Vyama vya Msingi Ushirika vya mkoa wa Mtwara na hivyo kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya kiushirika ndani ya Mkoa wa Dodoma.

Ziara hiyo inafanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia Mei 13 hadi 14, 2026 na kuwahusisha Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa, Wenyeviti wa CCM Wilaya Mkoani Dodoma, Sekretariti ya Mkoa CCM, Baadhi ya Makatibu wa Chama wilaya na Wenezi,, Makatibu, Makatibu Tawala Uchumi na Uzalishaji Viwanda na Biashara na Kilimo.


Share To:

Alex Sonna

Post A Comment: