Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi leo Mei 7, 2026, ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano wa Kimataifa unaowakutanisha Wadau wa Utalii Duniani chini ya Baraza la Usafiri na Utalii Duniani (WTTC) unaofanyika ndani ya meli ya Crystal Serenity inayosafiri kutoka bandari ya Sokhna kuelekea Alexandria nchini Misri.

Kupitia Mkutano huo Dkt. Abbasi amekutana na kufanya mazungumzo na Rais na Mtendaji Mkuu wa Baraza hilo Bi. Gloria Guevara, Waziri wa Zamani wa Utalii wa Mexico akiwa na Makamu Mwenyekiti wake Bw. Najib Balala, Waziri wa Zamani wa Utalii wa Kenya ambapo wamejadili masuala mbalimbali na namna Baraza hilo linavyoweza kusaidia kuendeleza Sekta ya Utalii nchini katika maeneo ya mafunzo, teknolojia na uwekezaji.

Mkutano huo umehudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Misri Meja Jenerali Richard M. Makanzo.
Share To:

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: