Na Mwandishi Wetu, Iringa
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Kakurwa, ameipongeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa utekelezaji wa Mradi Shirikishi wa Wasindikaji na Wazalishaji wa Maziwa (TI3P), akisema umekuwa chachu ya mageuzi katika sekta ndogo ya maziwa kwa kuongeza uzalishaji, kuimarisha mnyororo wa thamani na kuboresha maisha yawafugaji nchini.
Dkt. Bashiru alitoa kauli hiyo alipotembelea banda la TADB katika Maonesho ya 29 ya Wiki yaMaziwa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwembetogwa mkoani Iringa, ambapo alipokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kutoka kwa Mratibu wa TI3P, Joseph Mabula.
Alisema mafanikio yanayoonekana kupitia mradi huo yanadhihirisha umuhimu wa uwekezaji katika sekta ya mifugo, hususan sekta ndogo ya maziwa, ambayo imeendelea kuwa nguzo muhimu ya usalama wa chakula, lishe, ajira na uchumi wa wananchi wa vijijini.
"Wakati umefika kwa taasisi nyingine za kifedha kuona fursa zilizopo katika sekta ya mifugo na kuongeza nguvu katika utoaji wa huduma za kifedha kwa wafugaji kama ambavyo zimekuwazikifanya katika sekta nyingine za uzalishaji," alisema Dkt. Bashiru.
Aidha, aliwataka wadau wa maendeleo, taasisi za kifedha, wasindikaji wa maziwa na vyama vya ushirika kuimarisha ushirikiano ili kuongeza tija katika uzalishaji, ukusanyaji, uchakataji namasoko ya maziwa nchini.
Alisisitiza kuwa vyama vya ushirika vina nafasi kubwa katika kuwa unganisha wafugaji wadogo, kuwawezesha kupata pembejeo, huduma za ugani, mikopo na masoko yenye uhakika, jamboambalo ni muhimu katika kujenga sekta ya maziwa yenye ushindani.
Mafanikio ya mradi wa TI3P yanaonekana moja kwa moja kwa wanufaika wake. Mwenyekiti waChama cha Ushirika cha Wafugaji wa Ng’ombe wa Maziwa cha IDCOS LTD cha mkoani Iringa, Alex Nyalusi, alisema chama hicho kimepata mafanikio makubwa baada ya kuwezeshwa naTADB kupitia mradi huo kupata mkopo wa ng’ombe 25 wa maziwa.
Nyalusi alisema uwekezaji huo umeongeza uzalishaji wa maziwa kutoka wastani wa lita 700 hadi lita 1,000 kwa siku, hatua iliyoongeza mapato ya chama na wanachama wake 84.
Alisema kabla ya kupata uwezeshaji huo, wafugaji wengi walikuwa wakikabiliwa nachangamoto za uzalishaji mdogo na kipato kisichokidhi mahitaji yao, lakini hali imeanzakubadilika kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji na ubora wa mifugo.
"Leo hii wanachama wetu wanaona matokeo ya moja kwa moja ya mradi huu. Kipatokimeongezeka, uwezo wa kuhudumia familia umeimarika na ari ya kuwekeza katika ufugaji wakisasa imeongezeka kwa kiasi kikubwa," alisema Nyalusi.
Aliongeza kuwa chama hicho sasa kinaangalia hatua inayofuata katika kuongeza thamani yamaziwa kwa kuwekeza katika uchakataji wa bidhaa mbalimbali zitokanazo na maziwa.
"Tunatarajia kurejea TADB kuomba uwezeshaji wa kupata mitambo ya kuchakata maziwa ilikuanza kuzalisha mtindi na yoghurt. Hii itatusaidia kuongeza thamani ya maziwa yetu, kupanuasoko na kuongeza mapato kwa wanachama," alisema.
Pamoja na mafanikio hayo, Nyalusi alisema sekta ndogo ya maziwa bado inakabiliwa nachangamoto mbalimbali zinazohitaji kushughulikiwa ili kuongeza kasi ya ukuaji wake.
Alitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na uhaba wa wataalamu wa uhimilishaji, upungufu wamaafisa ugani, changamoto za upatikanaji wa malisho bora, magonjwa ya mifugo pamoja namiundombinu duni katika baadhi ya maeneo ya uzalishaji.
Wadau wa sekta ya maziwa wanaamini kuwa kuongezeka kwa uwekezaji katika uzalishaji, ukusanyaji, uhifadhi na uchakataji wa maziwa kutasaidia kuifanya sekta hiyo kuwa moja yanguzo kuu za uchumi wa mifugo nchini.
Mradi wa TI3P unaotekelezwa na TADB umeendelea kutajwa na wadau mbalimbali kama mojaya mifano ya uwekezaji wenye matokeo chanya katika sekta ndogo ya maziwa, kutokana na mchango wake katika kuwaunganisha wazalishaji na wasindikaji, kuongeza tija ya uzalishaji nakuinua ustawi wa wafugaji wadogo nchini.










Post A Comment: