Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga (Mb), ameliagiza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kushirikiana kikamilifu na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na Taasisi nyingine husika katika kushughulikia na kuondoa kero zote zinazosababishwa na mifumo ya utoaji vibali kwa shehena zinazoingia nchini.
Waziri Kapinga ametoa agizo hilo akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Waziri Salum alipokutana na Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Ashura Katunzi na ujumbe wake Mei 29, 2026 katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam, kufuatia kuibuka kwa changamoto zilizojitokeza wakati wa kuunganisha mfumo wa TANeSW wa TRA na mfumo wa OAS wa TBS na kusababisha usumbufu kwa baadhi ya wafanyabiashara.
Aidha, Waziri Kapinga amepongeza jitihada zinazoendelea kuchukuliwa baina ya TBS pamoja na TRA katika kuunganisha mifumo ya kielektroniki ili kurahisisha taratibu na kuongeza ufanisi wa utoaji wa vibali kwa shehena za mizigo inayoingia nchini.


Post A Comment: