Kulikuwa na kipindi maishani mwangu ambapo nilihisi maisha yangu yote yalikuwa yanaanguka mbele ya macho yangu. Nilikuwa nafanya kazi kwa bidii sana kwenye kampuni niliyokuwa nimeajiriwa.

Nilijituma, niliheshimu kazi yangu, na nilikuwa naamini uaminifu ndio ulikuwa unanifanya nisogee mbele. Ndiyo maana siku mambo yalipoanza kubadilika, sikuamini kabisa. Ghafla nilianza kusikia uvumi.

Mwanzoni nilipuuzia nikidhani ni maneno ya kawaida ya kazini. Lakini kadri siku zilivyopita, nilianza kugundua baadhi ya wafanyakazi walikuwa wakiniepuka. Wengine walikuwa wakinitazama tofauti kana kwamba kuna jambo baya nilikuwa nimefanya.

Kwa kweli nilichanganyikiwa. Siku moja niliitwa ofisini kwa meneja. Nilishtuka kusikia nikihusishwa na jambo ambalo sikuwa nimefanya kabisa. Kulikuwa na madai yaliyokuwa yanaenea kwamba nilikuwa nimehusika kwenye kosa lililoharibu imani ya kampuni.

Kilichoniumiza zaidi ni kuona hata baadhi ya watu niliokuwa na ukaribu nao wakianza kuniamini vibaya. Nilijaribu kujitetea, lakini ilionekana kama tayari watu walikuwa wameamua ukweli wao kuhusu mimi.SOMA ZAIDI.
Share To:

Post A Comment: