Na Mwandishi Wetu
WAWEKEZAJI sekta ya Mkonge kote duniani wameahidiwa mazingira rafiki yatakayowavutia kuwekeza hapa nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Balozi Waziri Salum amesema hayo hivi karibuni wakati akihitimisha ziara yake mkoani Tanga kwa kutembelea kiwanda cha sabuni na Tanga Sisal Spinning Mill kinachotengeneza bidhaa za Mkonge.
Balozi Salum pia amesisitiza kuwa Wizara ya Viwanda inaendelea kutekeleza maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kusimamia ufufuaji wa viwanda vilivyokufa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Saddy Kambona alibainisha mafanikio yaliyopatikana katika sekta hiyo tangu kuingizwa kwa zao la Mkonge nchini Mwaka 1892.
Kwa mujibu wa Kambona sekta ya mkonge ni miongoni mwa maeneo yanayochangia ajira za watanzania na pato la taifa.







Post A Comment: