Na Mwandishi wetu ..Arusha

Baada ya kupita miaka 42 tangu kufariki kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, Hayati Edward Moringe Sokoine, wananchi mkoani Arusha wameendelea kukumbuka na kuthamini mchango wake, wakisisitiza umuhimu wa uwajibikaji, mapambano dhidi ya rushwa na kilimo cha kufa na kupona.

Wakizungumza wakati wa maandalizi ya misa ya kumbukizi itakayofanyika Aprili 12 katika eneo la Monduli Juu, wananchi hao walisema Sokoine alijitofautisha kwa uongozi wa vitendo ulioweka mbele maslahi ya taifa.

Baadhi ya viongozi wa chama cha wazee wanaume Tanzania Joseph Laitatei makamu wa Rais wa chama hicho alisema Sokoine alikuwa kiongozi aliyesimamia haki bila kuyumba na hakuvumilia vitendo vya rushwa. Kwa upande wake, Cloud Gwangu alieleza kuwa kiongozi huyo alihamasisha kwa nguvu sera ya kilimo cha kufa na kupona, akilenga kujenga taifa linalojitegemea kwa uzalishaji.

Naye Abel Mollel Mwenyekiti  wa wilaya wa chama hicho alisisitiza kuwa uwajibikaji wa Sokoine unapaswa kuwa somo kwa viongozi wa sasa, huku Geoge Mwakalukwa akimtaja kama mfano wa uongozi wa uadilifu usio na hofu.

Aidha viongozi wa Chama cha Wazee Wanaume Tanzania wameipongeza familia ya Sokoine kwa kuendelea kuuenzi na kuudumisha kumbukumbu ya kiongozi huyo kila mwaka, wakieleza kuwa hatua hiyo inasaidia kizazi cha sasa na kijacho kujifunza misingi ya uongozi bora.

Katika kuenzi uzalendo wa Hayati Edward Moringe Sokoine, baadhi ya wananchi wameeleza namna walivyoguswa na uongozi wake wa kujitolea kwa taifa.

Akizungumza, Cloud Gwandu, mkazi wa Arusha, amesema Sokoine alikuwa kiongozi wa vitendo aliyethamini maslahi ya wananchi kuliko yake binafsi.

“Uzalendo wake ulikuwa wa kweli, alipambana na rushwa bila kuogopa na alihakikisha rasilimali za taifa zinawanufaisha wananchi wote. Viongozi wa sasa wanapaswa kujifunza kutoka kwake,” amesema Gwandu.

Ameongeza kuwa msisitizo wa Sokoine kwenye kilimo cha kufa na kupona ulikuwa sehemu ya uzalendo wake, kwani aliamini taifa lenye chakula cha kutosha lina uhuru wa kweli.

Kwa mujibu wa Gwandu, mfano wa Sokoine unaendelea kuwa somo muhimu kwa kizazi cha sasa katika kujenga uongozi wenye uwajibikaji na uadilifu.

Hayati Sokoine alifariki dunia Aprili 12 mwaka 1984 kufuatia ajali ya gari iliyotokea Dumila mkoani Morogoro.

Wananchi hao wameeleza kuwa licha ya kupita kwa muda mrefu, bado taifa lina kila sababu ya kuuenzi na kuutumia urithi wa Sokoine kama mwongozo wa kujenga uongozi bora, unaozingatia uwajibikaji, kupinga rushwa na kukuza kilimo kwa maendeleo endelevu.

















Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
رسالة أقدم

Post A Comment: