Na Munir Shemweta, WANMM

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imewasilisha Randama ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Bajeti kuu ya Serikali.

Akiwasilisha randama hiyo leo tarehe 23 Machi, 2026 jijini Dodoma, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo amesema wizara yake imejipanga kuendelea kutekeleza vipaumbele muhimu vinavyolenga kuboresha sekta ya ardhi, ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya upimaji wa ardhi, utoaji wa hati miliki, pamoja na kudhibiti migogoro ya ardhi nchini.

Ameongeza kuwa, katika mwaka wa fedha 2026/2027, wizara inalenga kuimarisha mifumo ya kidijitali katika usimamizi wa ardhi ili kuongeza uwazi, ufanisi na mapato ya Serikali. Aidha, juhudi zaidi zitaelekezwa katika kupanga, kupima na kumilikisha ardhi katika maeneo ya mijini na vijijini.

Uwasilishaji wa Randama hiyo ni hatua muhimu katika mchakato wa kupitia na kuboresha Bajeti ya Wizara kabla ya kuwasilishwa rasmi bungeni kwa ajili ya kujadiliwa na kupitishwa.

Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: