Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhandisi Maryprisca Mahundi, ameagiza Chuo cha Maendeleo ya jamii Uyole kupitia dhana ya ushirikishwaji jamii kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutaka kazi hiyo kuwa endelevu ndani na nje ya chuo
Mahundi amezungumza hayo wakati wa mahafali ya kumi na sita ya chuo cha maendeleo ya jamii CDTI uyole yaliofanyika viwanja vya michezo chuo cha maendeleo ya jamii Uyole na kusema licha ya siku kumi na sita za kupinga ukatili kufanyika lazima zoezi hilo likawe endelevu
Ameitaka jamii inayozunguka Chuo na kila mwanafunzi ni vema kila mmoja akawa mjumbe kupeleka elimu ya kupinga ukatili hasa wanaporudi nyumbani au katika sehemu za kazi.
Mahundi amesema ni mategemeo ya Wizara na Serikali kwa ujumla kuwa watumishi na wanafunzi wa Chuo hicho wataendelea kutimiza wajibu kwa kufanya kazi kwa bidii na kuendelea kuzingatia sheria,taratibu,kanuni na miongozo mbalimbali ya Kitaifa na kama wakifanya hivyo wataendelea kutoa wahitimu mahili na wenye maadili mema wanaoweza kushindana katika soko la ajira .
Amesema mustakabali wa Taifa lolote duniani unategemea sana mchango wa Taasisi za mafunzo katika kuandaa wataalamu mahili na wenye weredi ambao ndio chachu ya kuleta mageuzi ya kifkra na maendeleo jumuishi na endelevu katika jamii yoyote
Naibu Waziri Mahundi ameongeza kuwa Wizara inatambua mchango mkubwa uliotolewa na Chuo cha maendeleo ya jamii Uyole katika kuanda wataalamu wa maendeleo ya jamii ambao wanatoa mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa na kuwapongeza wakufunzi kwa kufanya kazi hiyo kwa uweledi.
Mhandisi Mahundi amesema katika kutekeleza dhana ya uanagenzi ,ubunifu na kusema kama zitatekelezwa vyema zitawawezesha wahitimu kuajiliwa kwa urais zaidi,kijiajili na kuajili wengine huku jamii inayozunguka Chuo hicho ikinufaika na mafunzo hayo.
Kwa upande wake Mkurugenzi anayesimamia vyuo vya Maendeleo ya jamii nchi kutoka Wizara ya Maendeleo ya jamii.jinsia na makundi maalumu Neema Ndoboka amesema vyuo vya maendeleo ya jamii nchini vimekuwa na mchango mkubwa na kwenda maeneo mbalimbali hapa nchini katika kwenda kuleta maendeleo hasa vijijini na mashirika mengine
Awali akisoma taarifa ya chuo hicho makamu mkuu wa chuo anaeshughulikia taaluma Spay Mwangomile amesema kwa ujumla nidhamu ya wanafunzi imekuwa ya kuridhisha uku wakifundishwa maadili mema,uadilifu na uwajibikaji popote watakapokuwa wakiwa kama mabalozi wa chuo hicho na kuwataka wanafunzi waliohitimu chuo hicho kuwa wabunifu
Jumla ya wahitimu 530 wanawake 272 na 258 wanaume wamehitimu katika mahafali ya Chuo hicho katika ngazi ya aatashahada na shahada.









Post A Comment: