‎Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Dkt. Lameck  Ng'ang'a Karanga amewapongeza Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL) na shirika lisilo la serikali AFRICAI kwa kuendelea kutekeleza ujenzi wa miradi Miwili (2) ya maji mmoja ukiwa  kata Mbulumbulu na mwingine Kata ya Baray. 

‎Mhe. Dkt Lameck ametoa pongezi hizo leo Desemba 12, 2025 ofisni kwake wakati akipokea taarifa ya maendeleo ya miradi ya maji  inayotekelezwa na wadau hao katika vijiji vya Kambi ya simba, Dumbechand, Mbuga Nyekundu pamoja na Geobaj 

‎Aidha serikali imewahakikishia wadau hao  kuwapa ushirikiano  kwa kutumia Mamlaka zake ikiwemo RUWASA ili huduma ya maji iwafikie wananchi popote walipo na kwa nyakati zote. 

‎Miradi hiyo ilianza Oktoba 2025 na inatarajiwa kumalizika mwishoni kwa mwezi Januari 2026 huku zaidi ya wananchi 2, l000 wanakadiriwa kunufaika    na miradi hiyo ambayo itamaliza tatizo la maji katika vijiji hivyo.

Share To:

Post A Comment: