
Na Oscar Assenga, Tanga
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhaman ametangaza kuunda kamati maalumu itakayochunguza sababu zilizosababisha uwanja wa CCM Mkwakwani kufungiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokuchezewa mechi.

Akizungumza na waandishi wa habari siku baada ya uwepo wa Taarifa za kufungiwa uwanja huo na TFF,Rajabu alisema kwamba tume hiyo itajumuisha kamati ndogo kutoka CCM,Maafisa wa TFF na baadhi ya wadau soka mkoa wa Tanga.

Alisema kwamba wameamua kufanya hivyo kutokana na kwamba waanaamini kuna uzembe ulijitokeza kwa wale ambao walipewa jukumu la kusimamia uwanja huo na kupelekea kukumbana na rungu hilo la TFF.

Aidha alisema kwamba ameshangazwa na hatua ya TFF kufungia uwanja huo kutokana na hivi karibuni waliufanyia marekebisho makubwa na kujiridhisha kwamba unaweza kutumika kwa ajili ya mashindano mablimbali ya ndani na nje ya hicho hivyo walishangazwa kuona taarifa hiyo.

“Nilikuwa nimesafiri nje ya mkoa wa Tanga kikazi lakini nimelazimika kuhairisha safari yangu ili niweze kushughulika tatizo hilo na ndio maana leo hiii nimefika hapa uwanja kujionea na kuzungumza nanyi wanahabari na kukubaliana na uamuzi wa TFF kwamba zipo dosari ambazo zinapaswa kurekebishwa na hili tutalifanyia kazi”Alisema

Katika hatoba yake fupi iliyojaa hekima alionyesha kutokuwa na imani na viongozi ambao wamepewa dhamana ya kusimamia uwanja hatua iliyopelekea kuwaita mbele ya wanahabari na wadau wengine watoe maelezo.
Awali akizungumza kabla ya mkaribisha Mwenyekiti huyo,Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Mfaume Kizito alisema kwamba uwanja huo ulikuwa kwenye hali nzuri lakini alishtushwa na uamuzi ambao ulichukuliwa na TFF kuufungia uwanja huo.

Pamoja na kauli hiyo Mwenyekiti wa CCM Mkoa alimtaka Meneja wa Uwanja wa CCM Mkwakwani Akida Machai aeleze nini ambacho kimepelekea uwanja huo kufungiwa licha ya kufanyiwa maboresho makubwa katika siku zilizopita.
Ambapo Meneja huyo alidai kuwa moja ya changamoto iliysababisha hali hiyo ni kutokuwepo na maji ya kutosha kutokana na chanzo cha maji kwenye uwanja huo kukauka na kupelekea nyasi za uwanja kukauka.
Alisema kwamba changamoto nyengine ni uwepo wa mchwa katika eneo lenye majani na hivyo kuwalazimu kutumia dawa ya kumwagilia na kufanikiwa kuwaondosha
Mwisho.

Post A Comment: