Na Mwandishi WETU, SINGIDA


Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu imeandaa kikao kazi cha siku 3 kilichowakutanisha Wakuu   vitengo vya Ufuatiliaji na Tathmini kwa  Mikoa 26 nchini kilichofanyika katika ukumbi wa KBH by Royal Village Hotel uliopo Mkoani Singida.


lengo la kikao ni kueleza umuhimu wa zoezi la Ufuatiliaji,  Tathimini na upimaji wa utendaji wa shughuli za Serikali katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Akizungumza  wakati akifungua kikao hicho Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji wa Serikali (Sehemu ya Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa) Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu,  Ndugu John Bosco Quman amesema lengo la kikao hicho ni kujenga uwezo kwa wataalamu hao ili kutekeleza zoezi la Ufuatiliaji, Tathimini na upimaji wa Utendaji wa shughuli za Serikali katika ngazi ya Mikoa na Halmashauri zote kupitia Wakuu wa Idara na  Vitengo.

Aidha kikao kimewashirikisha washiriki kutoka Mikoa 24 kati ya 26 ambao wamepitishwa katika dhana mbalimbali zinazohusiana na masuala ya ufuatiliaji, tathimini na upimaji utendaji wa  afua mbalimbali za Serikali  ukijumuisha sera,mipango mikakati ,miradi na Programu zinazotekelezwa kwenye ofisi za wakuu wa Mikoa na Halmashauri zote nchini.

"Msingi wa zoezi la ufuatiliaji na Tathimini kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ni kutokana na kuzingatia ibara ya 52 (1 ) ( 3) inayomkasimu madaraka Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa msimamizi mkuu wa Shughuli za Serikali siku hadi siku". Amesema Quman.

Ameongeza kwamba bado Serikali inaendelea kukamiikisha Sera ya Kitaifa ya Ufuatliaji na Tathimini Nchini ambayo ipo katika hatua za Uandishi baada ya kupita katika kamati ya Kitaifa ya uchambuzi wa Sera.


Hata hivyo amesema kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu imeendelea kuandaa taarifa za Utendaji wa Serikali ikiwemo taarifa ya 3 katika mwaka wa 2024/25 ambayo ipo katika hatua ya ukamilishaji na itawasilishwa hivi karibuni.

Pamoja na hayo Quman amesema kwamba, jitihada zinaendelea katika Mashirika ya Umma pamoja na Makampuni ya Serikali kuwa na Idara za Ufuatiliaji na Tathmini zinazojitegemea pia jitihada kubwa zimewekwa katika  ngazi ya Mikoa na  Halmshauri ili kuhakikisha vitengo hivi vinajitegemea na kutekeleza majukumu yake.


Hata hivyo Mkurugenzi Quman amesisitiza wajumbe walioshiriki kupitishwa kwenye mafunzo mahususi yanayotokana na muongozo jumuishi wa ufuatiliaji na tathimini wa Utendaji wa Serikali  wa mwaka 2023/24, pamoja na nyaraka nyingine ziwawezeshe kujua na kufuatilia Sera, Miradi, Mikakati, Mipango na programu mbalimbali katika maeneo yao.


Mwisho.

Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: