Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa, Ndg. Bulugu Magege, leo amefanya ziara katika Jimbo la  Makambako, akipita mtaa kwa mtaa kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo vituo vya abiria (vituo vya mabasi), migahawani, na vijiweni kwa lengo la kuwaomba wananchi waichague CCM.

Kila alipopita, vijana na wananchi walimhakikishia kwa shangwe kwamba tarehe 29 Oktoba 2025 watampigia kura Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Daniel Chongolo kwa nafasi ya Mbunge wa Jimbo la Makambako, pamoja na wagombea udiwani wa CCM kata zote za wilaya ya Njombe.

Bulugu aliambatana na viongozi wa UVCCM Wilaya ya Makambako, na alitumia ziara hiyo kuhimiza ari ya vijana kulinda na kusimamia kura za CCM. Aidha, alisisitiza kuwa Dkt. Samia ameendelea kuthibitisha kuwa ni Rais anayewapenda na kuwajali vijana, wakulima, na wafanyabiashara kwa kuwaletea maendeleo makubwa kupitia miradi ya elimu, barabara, umeme, na huduma muhimu za kijamii.

Share To:

Post A Comment: