Katibu wa NEC, itikadi, uenezi na mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Kenani Laban Kihongosi amesisitiza umuhimu wa amani Wilayani Busega Mkoani Simiyu pamoja na kujitenga kutumika kisiasa kwa ajenda za kuvuruga amani ya Tanzania hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu.
Kihongosi amebainisha hayo leo Alhamisi Oktoba 09, 2025 kwenye Viwanja vya Kituo cha Mabasi Lamadi, Wilayani Busega Mkoani Simiyu wakati wa Mkutano mdogo wa Kampeni za Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa Njiani kuelekea Mkoani Mara, akirejea vurugu baina ya wananchi na Vyombo vya ulinzi na usalama zilizotokea eneo hilo Agosti 2024 kutokana na kupotea kwa baadhi ya watoto katika eneo hilo.
"Wale waliowatuma kufanya vurugu hakuna hata familia moja iliyoumia ni imano yangu kuwa waliona madhara ya fujo. Niwaombe jambo moja Lamadi Mungu ametupa uhai tuulinde uhai tulionao na tusitumike kisiasa kubeba ajenda za uvunjifu wa amani madhara yake ni makubwa." Amesisitiza Kihongosi ambaye wakati huo alikuwa Mkuu wa Mkoa huo wa Simiyu.
Kihongosi pia amesisitiza kuhusu ulinzi wa amani, umoja na mshikamano wa Watanzania, akitaka siasa kutowagawa Watanzania na kuomba Wananchi wa Wilaya hiyo kumchagua kwa kura nyingi Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na wagombea Ubunge na Udiwani wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi itakapofika Jumatano ya Oktoba 29, 2025, siku ya uchaguzi mkuu wa Tanzania.
Post A Comment: