Na Denis Chambi, Tanga
KATIKA kuendelea kukabiliana na migogoro baina ya wakulima na wafugaji ambayo imekuwa ikileta athari mbalimbali katika jamii za wananchi wanaoishi wilaya ya Pangani mkoani Tanga shirika lisilo la kiserikali la Pangani Coastal Paralegal 'PACOPA' limeendelea kutoa elimu kwa jamii kwa lengo la kuleta amani.
Baada ya PACOPA kutoa elimu kwa makundi hayo na kutoa maadhimio ya kushirikiana kutokomeza migogoro pamoja na kufuata Sheria ikiwemo ya mpango wa matumizi bora ya ardhi zimeundwa kamati maalumu katika kata ya Bweni ambazo zitasaidia kusuluhisha migogoro pindi itskapotokea hatua ambayo inakwenda kupunguza malalamiko ambayo yamekuwa yakipelekwa katika ngazi za Halmashauri ya wilaya ya Pangani.
Elimu hiyo inayotekelezwa kupitia mradi wa Tujenge amani pamoja uliopo chini ya shirika la PACOPA kwa kushirikiana na We World pamoja na shirika la Twaweza imeanza kuleta matokeo chanya baada ya jamii hizo za wakulima na wafugaji kukiri mabadiliko waliyonayo sasa baada ya kupatiwa elimu hiyo.
Mathayo Madeleke pamoja na Saumu Bakari ambao ni wa kulima kutoka katika kata ya Bweni wameeleza manufaa waliyoyapata kupitia elimu hiyo waliyopatiwa ambapo wameahidi kwenda kuwa mabalozi kwa wananchi wengine.
Wamelishukuru shirika la PACOPA kwa kushirikiana na we World pamoja Taweza kuwa kuwafikishia mradi huo wenye lengo la kutoa elimu ya matumizi bora ya ardhi pamoja na kujenga amani na mshikama o baina yao.
"Tunawashukuru sana wahisani waliotuletea mradi huu tulikuwa tukiingia kwenye migogoro mbalimbali lakini shida ni elimu tuliyokuwa nayo kuhusu Sheria zinazonekana zimepitwa na muda sana , tulikuwa tunaomba elimu iendelew kutolewa ili tuweze kujenga amani hii tuliyonayo hii itatusaidia kuelimiahana sisi kwa sisi binafsi naahidi kwenda kuwa balozi kwa wengine kuhusu elimu hii nipiyoipata
Alfred Mwalongo ambaye ni mfugaji kutoka kata ya Bweni ameeleza kuwa migogoro mingi inayotokea baina ya jamii hizo imekuwa ikisababishwa na wafugaji kutokana na kutokufuata Sheria zilizopo wengi wakitafuta malisho ya mifugo yao hata maeneo ambayo hayajaruhusiwa jambo ambalo limekuwa likisababisha kutokuolewana baina yao na wakulima.
"Ukweli semina hii imetuelimiaha sehemu kubwa husasani sisi wafugaji ambao tulikuwa tunaishi kwa mazoea kutokana na utamaduni ambao tulikuwa nao tukiamini kuwa popote pale tunaweza kwenda kulisha mifugo yetu, lakini sasa tunaoaswa kufuata Sheria bila ya kuwa wakaidi kwa sababu kwa kufanya hivyo ni kudumaza maendeleo wakulima na wafugaji tunategemeana Kila siku"."
Mratibu msaidizi wa mradi wa kujenga amani kutoka shirika la Pangani Coastal Paralegal 'PACOPA' Mwanakuzi Abdillah amesema kuwa lengo lao ambalo limejikita zaidi katika kuhamasisha wananchi kushiriki Moja kwa moja kwenye utatuzi wa migogoro pale inapotokea kwa kushirikiana na wadau pamoja na viongozi wa Serikali kuanzia ngazi za vijiji.
Ameongeza kuwa kutokana na elimu waliyoitoa kupitia mradi huo uelewa kwa jamii katika kutatua migogoro baina ya wafugaji na wakulima umeongezeka hatua ambayo inakwenda kuleta mabadiliko kwao na hatimaye kufikia lengo la mradi huo wa kujenga amani na kutokomeza kabisa migogoro.
"Lengo kubwa la mradi huu ni kuongeza ushiriki wa wananchi katika kutatua changamoto zao wenyewe ili kuepusha migogoro katika mradi huu wa kujenga amani tunaamgalia zaidi ni jinsi Gani wananchi wao wenyewe wanaweza tutatua migogoro kwa kushirikiana na wadau pamoja na viongozi wa Serikali zao za vijiji"
"Baada ya kuleta mradi huu tumeona kuwa jamii zimekuwa na uelewa zaidi katika kutatua migogoro hata zile kesi za mapigano Kati ya wakulima na wafugaji zimepungua katika kata ya Bweni wengi wamekuwa wakikimbilia katika Serikali zao za vijiji kurlezea zile changamoto walizonazo na kupata utatuzi"
Mratibu hiyo amebainisha kuwa kumekuwa na uelewa mdogo kwa jamii za wakulima na wafugaji hasa kwa namna ya kusuluhisha na kutatua migogoro yao ambapo wengi wamekuwa wakijichukulia Sheria mkononi lakini baada ya mradi huo kumekuwa na mabadiliko chanya hasa.
Post A Comment: