DENIS MLOWE, NJOMBE
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Makete Festo Sanga kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) anatarajiwa kuzindua rasmi kampeni zake Septemba 14 kuwania kuchaguliwa na wananchi katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka mwaka huu huku mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Aliyekuwa Spika wa Bunge Tulia Ackson.
Festo Sanga ambaye amejipambanua kuwa mmoja wa wabunge waliotoa mchango mkubwa katika bunge lililopita licha ya Tulia atasindikizwa na viongozi mbalimbali wa Chama na wasanii wa ndani na nje ya mkoa wa Njombe.
Akizungumza na mwanahabari hizi Sanga alisema kuwa Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Makete Stend huku akisindikizwa na msanii Rayvanny Sambamba na B2K kutoka Makambako.
Alisema kuwa baada ya uzinduzi rasmi wa mgombea wa Urais mkoani Njombe sasa mbio za ubunge zinaanza rasmi hivyo wananchi wajitokeze kusikia ahadi mbalimbali ambazo ziko katika ilani ya CCM 2025 hadi 2030 zenye kumletea maendeleo mwananchi.
Sanga mbunge kijana mwenye hoja nzito bungeni alisema kuwa wananchi watapata burudani na kisha kupewa dozi ya mambo makubwa waliyofanyika na serikali ya CCM katika jimbo la Makete.
"Tunazindua rasmi kampeni za chama chetu, tunakaribisha vyama vyote kuja kusikiliza sera zetu na Ilani ya Uchaguzi ya chama chetu iliyobeba matumaini, iliyobeba sekta zote na kutoa majawabu ya changamoto zilizoko ndani ya jimbo,” alisema.
Alisema kuwa atawanadani madiwani wa kata zote katika jimbo hilo ambapo uzinduzi utaanza saa 3 asubuhi katika viwanja hivyo.
Alisisitiza kwamba kampeni za chama hicho zitakuwa za kistaarabu zikibeba misingi ya kulinda amani, utu na taifa na tutakwenda kufanya kampeni kwa kutumia hoja, hakutakuwa na matusi, hatutatweza au kudhalilisha utu wa mtu mwingine ndani ya jimbo la Makete.
Post A Comment: