Katika kijiji kimoja wilayani Tarime, aliishi kijana aitwaye Emmanuel. Tofauti na watoto wengine, Emmanuel hakuwa kijana mwenye akili ya kung’aa darasani. Mara zote alipopewa mitihani, jina lake lilikuwa likiorodheshwa nafasi ya mwisho. Walimu wake walijitahidi kumsaidia, lakini bado hakufaulu. Wanafunzi wenzake walimcheka kila mara wakimwita majina ya kubeza kama “kichwa maji” au “mjinga wa darasa.”
Hali hiyo ilimvunja moyo sana, lakini hakuweza kufanya chochote. Hatimaye, alipoifikia darasa la saba, matokeo yake yalikuwa mabaya sana kiasi cha kutofanya vizuri mtihani wa kumaliza shule ya msingi. Ndoto zake za kuendelea na masomo zilikatika ghafla. Wazazi wake walihuzunika, lakini kwa kuwa walikuwa maskini, hawakuweza kumsaidia kwa njia nyingine zaidi ya kumshauri akae nyumbani na kusaidia kazi za shamba.
Emmanuel alikaa nyumbani kwa muda, akiwa na mawazo tele. Aliona kila siku wenzake waliokuwa wakifanya vizuri darasani wakichaguliwa kuendelea na sekondari, huku yeye akibaki nyuma. Machozi yakawa chakula chake cha kila siku. Lakini moyoni, kijana huyu hakuwa amekata tamaa kabisa. Alianza kufuga kuku wachache aliopewa na mama yake kama njia ya kujifariji.
Kuku wale walianza kuongezeka, na polepole akapata fedha ndogo za kujikimu. Lakini bado, biashara yake haikuwa kubwa sana. Wakati mwingine magonjwa yaliwapiga kuku wake na kumpotezea matumaini. Soma zaidi hapa
Post A Comment: