DKT. SAMIA: MAFANIKIO 



Mgombea wa nafasi ya Rais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta mbalimbali za maendeleo nchini ni matokeo ya matumizi sahihi na usimamizi imara wa mapato yanayotokana na kodi za wananchi na mikopo.

Akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo, Septemba 10, 2025, wilayani Nzega mkoani Tabora, Dkt. Samia amesema usimamizi huo umewezesha pia kukabiliana na tatizo la rushwa nchini.

Dkt. Samia amebainisha kuwa iwapo kusingekuwepo na usimamizi thabiti wa fedha hizo, miradi mbalimbali mikubwa ya maendeleo isingeonekana leo. Alisisitiza kuwa kazi kubwa imefanyika kuhakikisha kila shilingi ya mapato ya serikali inatumika kwa faida ya Watanzania.

Vilevile, ametaja tafiti za mashirika ya ndani na kimataifa zinazobainisha kuwa viwango vya rushwa nchini vimeendelea kupungua, jambo linaloashiria ufanisi wa jitihada zinazofanywa na serikali ya CCM.

Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: