Yona alikuwa kijana mnyenyekevu na mwenye heshima kubwa katika kijiji chao kilichopo Kagera. Alikuwa mchapakazi, akijishughulisha na biashara ndogo ndogo za kuuza vifaa vya nyumbani sokoni. Kwa umbo na tabia, Yona hakuwa mtu wa mabishano au kelele nyingi. Ndoto yake kubwa ilikuwa moja tu: kupata mwenzi wa maisha ambaye angempenda kwa dhati na kushirikiana naye katika safari ya maisha.

Katika siku zake za kawaida sokoni, alikutana na binti mrembo aliyeitwa Anna. Anna alikuwa na tabasamu lililong’aa na sura ya kuvutia kiasi kwamba kila kijana kijijini alitamani kumkaribia. Kwa Yona, haikuwa tu urembo wa sura bali pia moyo wake ulihisi kuwa huyu ndiye mwanamke aliyekuwa ameumbwa kwa ajili yake. Tangu siku hiyo ya kwanza, moyo wa Yona ukamwambia: “Anna ndiye mke wangu wa baadaye.”

Lakini safari haikuwa rahisi. Yona alianza kumfuata Anna, akimweleza hisia zake na kumwomba wawe wapenzi. Kwa bahati mbaya, kila mara Anna alikuwa akitoa majibu ya kumkataa. Wakati mwingine alitabasamu na kumwambia:

“Yona, bado sijawa tayari.”

Wakati mwingine alitoa ahadi zisizo na uhakika:

“Ngoja kwanza, nitakujibu kesho.”

Lakini kesho ilipowadia, Anna hakuwa akisema lolote. Mwaka ukapita, na mwaka mwingine ukaingia. Yona hakuacha, aliendelea kumsumbua kwa heshima na upole. Mapenzi yake yalikuwa ya dhati, lakini Anna hakuwa tayari kuyakubali. Soma zaidi hapa 

Share To:

contentproducer

Post A Comment: