Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, amekutana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya DL Group, Ndugu Dr. David Langat, pamoja na viongozi wa wafanyabiashara kutoka mkoa wa Njombe.
Katika kikao hicho walihudhuriwa na wadau kutoka taasisi mbalimbali za mkoa, pamoja na vikundi vya uwakilishi kutoka kwa wanawake.
Kikao Hicho Kilijikita katika kujadili fursa za uwekezaji katika viwanda, na namna ambavyo sekta hii itakavyoinua uchumi wa wananchi wa Njombe. Fursa za uwekezaji zilijikita katika zao la parachichi, chai, na viazi, ambapo kupitia uwekezaji katika viwanda vya usindikaji, kuna matumaini ya kuongeza mnyororo wa dhamani wa mazao haya na kuleta manufaa kwa wakulima na wajasiriamali wa eneo hili.
Mhe. Mtaka alisisitiza umuhimu wa kushirikiana na sekta binafsi ili kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi wa Njombe, huku akitaja kuwa uwekezaji huu utasaidia kuongeza ajira, kuboresha miundombinu, na kukuza sekta ya kilimo. Wadau walieleza matumaini yao kwamba hatua hizi zitakuza uchumi wa mkoa na kuboresha hali ya maisha ya wakazi wake.
Post A Comment: