Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Arusha aliyemaliza muda wake,Mheshimiwa Cecilia Paresso akimwombea kura mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dkt.Samia Suluhu Hassan na wagombea ubunge wa chama hicho mkoa wa Manyara uliofanyika viwanja vya Motel Papa mjini Babati
Aliyekua mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Arusha,Mheshimiwa Cecilia Paresso akimwombea kura mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dkt.Samia Suluhu Hassan na wagombea ubunge wa chama hicho mkoa wa Manyara uliofanyika viwanja vya Motel Papa mjini Babati. 

Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Arusha aliyemaliza muda wake,Mheshimiwa Cecilia Paresso (kulia)akipongezwa na mgeni rasmi wa ufunguzi wa kampeni za uchaguzi mkuu mkoa wa Manyara,Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,Hamad Chande baada ya kumwombea kura mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dkt.Samia Suluhu Hassan na wagombea ubunge wa chama hicho mkoa wa Manyara uliofanyika viwanja vya Motel Papa mjini Babati,kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Manyara,Peter Toima.
Wagombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Manyara wakiwa katika mkutano huo.

 Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mratibu wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi(CCM) Kanda ya Kaskazini akifurahia jambo na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Arusha aliyemaliza muda wake,Cecilia Paresso mjini Babati mkoa wa Manyara.

Wakazi wa mjini Babati wakifurahia hotuba zilizokua zikitolewa kwenye mkutano wa kampeni kuwanadi wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)mkoa wa Manyara.
Wakazi wa mjini Babati wakifurahia hotuba zilizokua zikitolewa kwenye mkutano wa kampeni. 


Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Arusha aliyemaliza muda wake,Mheshimiwa Cecilia Paresso ameendelea kueleza utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi kilichopita akiomba kura za wananchi wa mkoa wa Manyara kumwamini kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Paresso ambaye anajukumu la kumtafutia kura mgombea wa urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mikoa wa Kanda ya Kaskazini na wabunge wa chama hicho,ametamba kuwa fedha nyingi zilizoelekezwa kwenye miradi ya maendeleo inazungumza yenyewe na wananchi kwenye halmashauri za mkoa huo wameona mabadiliko makubwa.

Ametaja ujenzi wa Shule mpya za Msingi na Sekondari mkoa wa Manyara umewapunguzia changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kutafuta elimu huku wasichana wakiingia kwenye vishawishi ambavyo vinaweza kukatisha ndoto zao za kufikia malengo ya kielimu.

"Tumeshuhudia Rais Samia alivyoelekeza mabilioni ya fedha kwenye sekta ya elimu na mabadiliko ya sera ya elimu inayowawezesha wasichana waliopata changamoto ya kupata ujauzito wakiwa bado shule kuendelea na elimu ili kufikia malengo yao"amesema Paresso.

Mheshimiwa Paresso ameshafanya mikutano ya kumwombea mgombea urais wa CCM,Dkt.Samia Suluhu Hassan wilaya ya Karatu na Arumeru mkoa wa Arusha,wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro na Babati mkoa wa Manyara.

Ameongeza kuwa Rais Samia ameahidi kufufua mchakato wa Katiba Mpya ndani ya Siku 100 za uongozi wake baada ya kuchaguliwa madai ya muda mrefu ya wadau mbalimbali wa kisiasa na taasisi za kiraia.

"Mheshimiwa Rais Samia ni msikivu bila kujali waliokua wanapigania mabadiliko ya Katiba Mpya ameahidi ndani ya muda mfupi baada ya kuchaguliwa ataongoza mchakato wa kuwapatia Katiba Mpya,kwahiyo wale ambao wapo kwenye vyama vya upinzani wamuunge mkono kwa kumpigia kura za kishindo na wajiunge na CCM,"amesema Paresso


 

Share To:

Post A Comment: