Na Denis Chambi, Tanga.


HALMASHAURI ya Wilaya ya Pangani imezipongeza kamati za waraghibishi zinazofanya kazi ya kuibuka na kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika maeneo yao hatua ambayo imesaidia  kuongeza ushiriki wa wananchi katika kujiletea maendeleo ikiwemo kukomesha vitendo vya ukatili ambavyo  vimepungua kwa kiasi kikubwa.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo kwa kamati hizo yaliyoshirikisha waandishi wa habari, mkuu wa  idara ya  maendeleo ya jamii kutoka katika halmashauri hiyo Sekela Mwalukasa amesema kuwa  uwepo wao umewezesha pia kutekeleza miradi na kazi mbalimbali ambazo zipo kwenye mpango wa Serikali ila kupitia waraghibishi hao waliopo katika ngazi ya vijiji  wameweza kuhamasishana na kuunga mkono juhudu za kutatua  changamoto zilizopo ikiwemo kwenye sekta ya elimu , miundombinu, na afya. 

"Matokeo tuliyoyapata kupitia kamati hizi mpaka sasa ni makubwa kwa sababu wameweza kufikia zile kazi ambazo Serikali ilipaswa kuzifanya ili wao kwa umoja wao wanaweza kuhamasishana na kuzifanya bila kuisubiri Serikali Kuna baadhi ya vijiji wananchi walikuwa na muamko mdogo wa kushiriki kwenye shughuli za maendeleo lakini kupitia huu urakibiahi tumeona matunda yake"


"Tunawaomba sana   wananchi kupitia hizi kamati za urakibiahi wawe na uhuru popote pale wanapoona kuna changamoto ni vyema wakazitatua kwa haraka ili kuepuka migogoro ambayo inaweza kujitokeza mbeleni lakini pia hata yale mazuri ambayo yanaweza kuleta hamasa ya maendeleo waweze kuyaibua" alisema Nsekera.

Mratibu wa uraghibishi kutoka shirika la Pangani Coastal Paralegal 'PACOPA' Mtumwa Kombora amesema kuwa pamoja na shughuli ambazo wamezifanya kwa mafanikio makubwa bado  ushirikiahwaji wa wananchi katika shughuli za maendeleo ni mdogo hivyo kuiomba Serikali kupitia viongozi wa vijiji kushirikiana kwa karibu na Wananchi.


"Mpaka sasa kupitia Waraghibishi hawa kuna mambo mazuri yamefanywa na tunatamani yafike mbali katika maeneo mengine tunaomba  na tunatamani kuona Serikali inaboresha mahusiano yao na wananchi , mwananchi anapaswa kushiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo lakini kiongozi ana nafsi ya kumshirikisha mwananchi katika namna yote Ile" amesema Kombora.


Kwa upande wake Happynes Mkwera kutoka shirika la TWAWEZA amesisitiza juu umuhimu wa dhana ya ushiriki wa wananchi katika kuibua changamoto zilizopo na kutafuta namna bora ya kuzitatua kupitia viongozi wao wa Serikali ya vijiji.


Mkwera ameongeza kuwa  tangu kuanza kwa Kamati hizo ndani ya wilaya ya Pangani kumekuwa na mabadiliko makubwa hususani kwa jamii  jambo ambalo linaleta matokeo chanya kupitia mradi huo. 


"Katika hivi vijiji ambavyo tunafanyia kazi tunaona kuna mabadiliko makubwa hususani katika utekelezaji wa vipaumbele ambavyo vimechaguliwa na wananchi wenyewe ambapo utekelezaji unaendelea na waraghibishi wamekuwa wakifanyia kazi na kwa hatua tuliyofikia sasa tunaona angalau ushiriki wa wananchi unaendelea kukua siku hadi siku lakini pia hata viongozi kuwajibika kwa wananchi" amesema Mkwera.


Baadhi ya wananchi waliopo katika kamati hizo  wamepongeza mradi huo unaosimamiwa na shirika la Pangani Coastal Paralegal 'PACOPA' kwa kushirikiana na Shirika la TWAWEZA katika ngazi ya vijiji hii ni kutokana na mafanikio waliyoyapata tofauti na hapo awali.

Share To:

OSCAR ASSENGA

Post A Comment: