Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi (katikati), akitizama bidhaa katika kiwanda darasa, wakati wa ziara tarehe 13 Agosti 2025. na Makamu Mkuu wa Taasisi, Profesa Maulilio Kipanyula (kulia), akiwa na Rose Mosha, Meneja Mradi (kushoto)

Na.Mwandishi Wetu.

Halmashauri nchini zimeshauriwa kujifunza na kutumia teknolojia ya mashine ya kisasa ya kuchakata uchafu na kuzalisha mbolea na gesi asilia ubunifu kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) kwa lengo la kuboresha usimamizi wa taka na kuongeza fursa za ajira kwa vijana, wanawake, na watu wenye mahitaji maalum

Wito huu umetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi, tarehe 13 Agosti, 2025, alipotembelea taasisi hiyo Mhe. Chumi ameeleza kuwa halmashauri zinaweza kutumia asilimia 10 ya fedha zinazotolewa na Serikali kwa makundi haya kuunda vikundi vitakavyotumia teknolojia hiyo kuchakata taka na kuzalisha mbolea kwa matumizi ya wakulima

“Mbolea hii itakuwa chanzo cha ajira kwa wananchi na wakati huo huo kusaidia halmashauri kudhibiti taka katika maeneo yao,” alisema Mhe. Chumi

Aidha, Mhe. Chumi alisisitiza kuwa ubunifu na tafiti zinazofanywa katika taasisi hiyo zina mchango mkubwa si kwa Tanzania pekee bali pia kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kupitia utekelezaji wa sera za mambo ya nje hususan diplomasia ya uchumi

Pia, alibainisha kuwa wizara yake itaendelea kushirikiana na balozi wa Tanzania nje ya nchi ili kuwezesha taasisi kama NM-AIST kupata wanafunzi na wahadhiri wa kimataifa Hii itasaidia kuongeza uwezo wa kitaalamu na kusambaza ubunifu hizo kimataifa

Mhe. Chumi alihimiza taasisi hiyo kushiriki katika maonyesho ya kimataifa ili kuvuka mipaka ya kitaaluma na kibiashara Alisema wizara iko tayari kushirikiana na taasisi katika matukio ya kimataifa ili kuhakikisha ubunifu wa Tanzania unatambulika duniani

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa NM-AIST, Prof. Maulilio Kipanyula, amesema taasisi hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kuzalisha teknolojia na hivi karibuni ilipokea tuzo ya kuwa taasisi kinara katika usajili wa hakimiliki

“Tuzo hii ni ishara ya kuwa bunifu zetu zina nafasi kubwa sokoni Hata hivyo, kufanikisha hilo kunahitaji ushirikiano wa wadau mbalimbali, ikiwemo Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,” alisema Prof. Kipanyula

Profesa Kipanyula pia alibainisha kuwa taasisi imeanza kutekeleza mikakati ya kuwafikia wadau wa ndani na wa nje ya nchi Kwa upande wa wadau wa ndani, taasisi imeanza kufanya uwasilishaji wa mawazo ya biashara kwa kuwatembelea wadau ili waweze kuzifahamu na kufanya uthibitishaji wa ubora Mfano wake ni mkoa wa Njombe kupitia bidhaa kama uji tayari pamoja na Kampuni ya Kamal kwa ajili ya kubiasharisha baadhi ya bunifu hizo Hatua inayofuata ni kupeleka teknolojia hizo nje ya nchi

Aliongeza kuwa taasisi imejikita katika kutafuta majawabu ya changamoto mbalimbali zinazolikumba bara la Afrika kupitia utafiti na ubunifu unaolenga kuhudumia jamii na viwanda

 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi, akipata maelezo kutoka kwa Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Profesa Maulilio Kipanyula, wakati wa ziara yake katika taasisi hiyo

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi (katikati), akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Utafiti na Ubunifu, Prof. Thomas Kivevele (wa kwanza kushoto). Kulia ni Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Profesa Maulilio Kipanyula,  wakati wa ziara yake.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi (katikati), akitizama bidhaa katika kiwanda darasa, wakati wa ziara tarehe 13 Agosti 2025. na Makamu Mkuu wa Taasisi, Profesa Maulilio Kipanyula (kulia), akiwa na Rose Mosha, Meneja Mradi (kushoto)

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi (wa kwanza kushoto), akipata maelezo kuhusu ubunifu wa chanjo ya samaki kutoka kwa Sylvester Temba (kulia), wakati wa ziara tarehe 13 Agosti 2025. Wa pili kushoto ni Makamu Mkuu wa Taasisi, Profesa Maulilio Kipanyula.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi (aliyekaa), akiangalia jinsi elimu ya kidigitali inavyofanya kazi wakati wa ziara yake katika Kituo cha Elimu Kidigitali (C-CoDE) cha Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela. Pamoja naye ni Makamu Mkuu wa Taasisi, Profesa Maulilio Kipanyula (kulia), Mkuu wa Kituo cha Umahiri WISEFuture, Profesa Hans Komakech (wa kwanza kushoto), na Afisa Tehama wa Kituo, Bw. Octavian Kanyengele (wa pili kushoto).

 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi (kushoto), akipokea zawadi ya kumbukumbu kutoka kwa Makamu Mkuu wa Taasisi, Prof. Maulilio Kipanyula (kulia), wakati wa ziara

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela mara baada ya ziara yake.

Share To:

Post A Comment: