Video inayotrend kwenye TikTok imezua maoni mengi tofauti baada ya kuonyesha sherehe ndogo ya harusi kati ya mwanamke mwenye umri unaokadiriwa kuwa miaka hamsini na kijana anayekadiriwa kuwa na miaka ishirini na moja, tukio lililowavutia na kuwashangaza watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii.
Katika video hiyo, wanandoa hao wanaonekana wakiwa wamependeza, wameshikana mikono huku wakitazamana kwa tabasamu la dhati, ishara kwamba penzi lao limejaa furaha na matumaini.
Watu waliokuwa wamezunguka eneo hilo walionekana kushangilia na kupiga makofi, ishara ya kuunga mkono hatua waliyochukua. Mmoja wa watumiaji wa TikTok alitoa maoni akisema, “Hii inathibitisha kuwa mapenzi ni moyo, si tarehe ya kuzaliwa.” Soma zaidi hapa
Post A Comment: