Jina langu naitwa Farida mkazi wa mkoa wa Katavi, umri wangu ni miaka 38, nipo kwenye maisha ya ndoa miaka 10 sasa na mume wangu Yazidi, tulifunga ndoa ya kimila ambayo ilihudhuriwa na wazazi wa pande zote mbili.

Baada ya kuolewa mume wangu alinifungulia biashara ya kuuza nguo kwa ajili ya kuweza kujipatia fedha ndogo ndogo kwa ajili ya kujinunulia baadhi ya vitu kama mama wa nyumbani.

Nilijituma kadiri ya uwezo wangu kuendesha biashara ile vizuri na Mungu aliniwekea mkono wake, kila siku nilikuwa natengeneza faida na siyo hasara.

Siku zilipita na hatimaye nikapata ujauzito, hivyo ikanibidi nitafute mtu wa kunisaidia kazi nyumbani hata dukani pia, katika harakati za kutafuta mtu wa kunisaidia kazi, mume wangu aliweza kumpata msichana kutoka kijijini kwao.

Msichana huyo aliitwa Swaum, mara moja alianza majukumu yake ya kila siku pale nyumbani na hata dukani alikuja kunisaidia mara chache. Soma zaidi hapa 

Share To:

contentproducer

Post A Comment: