SAMIA AAHIDI VITUO VYA AFYA NA ZAHANATI MPYA CHAMWINO
Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kuimarisha zaidi huduma za kijamii katika Jimbo la Chamwino ikiwa ni pamoja na afya, maji na barabara.
Akizungumza leo, Agosti 31, 2025, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Chamwino, mkoani Dodoma, Dkt. Samia amesema serikali ya CCM ina dhamira ya kuhakikisha wananchi wa jimbo hilo, ambalo pia ndilo lina Ikulu ya Rais, hawakabiliwi na changamoto za huduma za msingi.
Kuhusu upatikanaji wa maji, Dkt. Samia amesema: “Ninajua tuna shida ya maji, mgombea ubunge hapa amesema mradi mkubwa upo, ninataka niwahakikishie tutahakikisha Chamwino yote inapata maji kwa karibu zaidi.”
Aidha, ameahidi kuendeleza ujenzi wa miundombinu ya barabara, akisema serikali itajenga kilomita 10 za barabara za kiwango cha lami na kuimarisha barabara za changarawe katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.
Post A Comment: