Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ismail Ali Ussi amezitaka Taasisi za elimu nchini wakiwemo VETA kuhakikisha wanatunza mazingira sambamba na uoteshaji miti katika maeneo yao hayo yamejiri wakati wa ukaguzi wa mradi wa kuhifadhi mazingira na upandaji wa miti katika Chuo cha VETA Longido.
Ussi alisisitiza taasisi za elimu ikiwemo shule za msingi na sekondari kutunza mazingira ikiwemo upandaji wa vitalu vya miche ya aina mbalimbali ili kuhakikisha maeneo yaliyopo yanakuwa na uoto wa asili ikiwa ni kampeni ya Rais Samia Hassan Suluhu ya kuhakikisha Tanzania inakuwa ya kijani
"Endeleeni kupanda miti ili kuhakikisha Tanzania inakua ya kijani ikiwemo kuhakikisha vitalu vua miti ya aina mbalimbali lakini napongeza VETA kwa kuanzisha mradi huu unaowapa fursa za ajira vijana"
Awali akisoma taarifa ya mradi huo,Ofisa Ufugaji Nyuki halmashauri ya Longido,Remna Rombola alisema jumla ya miti 1000 imepandwa ikiwemo miche ya vitalu 8,000 ambayo imepandwa kwa gharama ya sh, milioni 4.3 ambapo halmashauri ya Longido imetoa sh, milioni 1.5 huku miti 1000 ikitolewa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)
"Mradi huu utasaidia unoreshaji wa mazingira kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo upunguzaji wa hewa ukaa"
Awali Mkuu wa Wilaya ya Longido Salum KalLi amesema mwenge wa Uhuru ukiwa wilayani hapo utakimbizwa kilomita 222.4 na kupitia jumla ya miradi saba ya bilioni 2.2
Post A Comment: