Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ismail Ali Ussu ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Serikali, kupitia Wakala wa Barabara za  Mijini na Vijijini (TARURA), kwa kutoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya  miundo ya barabara nchini, licha ya kurahisisha usafiri imechochea kasi ya maendeleo na kukuza uchumi katika maeneo mengi.

Akizungumza wakati akiweka Jiwe la Msingi mradi wa ujenzi wa Daraja la zege na chuma barabara ya Usa River - Maji ya Chai halmashauri ya Meru, daraja lililojengwa na  kwa gharama ya shilingi milioni 499.8,ameipongeza TARURA Arumeru kwa kazi nzuri waliyoifanya inayoakisi dhamira njema ya Mhe.Rais.

Kupitia mradi huo, Kiongozi huyo amesema kuwa, Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi mahiri wa Dkt.Samia Suluhu Hassan, imefanya kazi nzuri katika sekta zote ikiwemo miundo mbinu ya barabara na wilaya ya Arumeru ni moja ya eneo lililonufaika sana kwa kuzingatia miradi mingi iliyotekelezwa kwa kipindi cha awamu ya sita

"Nimeishuhudia kazi nzuri ya ujenzi wa daraja hili la mawe na chuma, daraja ambalo limejengwa kwa kuzingatia viwango vya ubora vinavyoenda na thamani ya fedha zilizotolewa na tayari limeanza kuwahudumia wananchi wa maeneo haya, ninaipongeza sana TARURA kwa kazi hii nzuri". Amesema

Ameongeza kuwa, kupitia mradi huu,  Mwenge wa Uhuru umeleta matumaini mapya kwa wananchi wa halmasahuri ya Meru, wananchi wamepata furaha na amani, kwa kuwa timu imejiridhisha daraja hilo limejengwa kwa ubora wa hali ya juu.










Share To:

Post A Comment: