Na, Egidia Vedasto, Msumba News

Wawekezaji wa ndani wameendelea kuchochea ukuaji wa sekta ya utalii na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Smia Suluhu Hassan, inayotaka taifa kufikia uchumi mkubwa ifikapo mwaka 2050.

Akizungumza na Wanahabari katika maonyesho ya msimu wa tano wa Karibu Kili Fair 2025 katika banda lake la maonyesho Mkurugenzi Mtendaji wa Heritage Camps and Lodges Collection Erick Mashauri amesema, Sekta ya Utalii ni muhimu katika mustakabali wa kuinua uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla. 

Aidha ameongeza kuwa ana mpango wa kuwekeza hoteli ya nyota tano katika mbuga ya Serengeti ya vyumba takriban 50, hatua itakayochochea ukuaji wa uchumi na kuzalisha ajira nyingi kwa vijana. 

"Huduma zetu ni nzuri na tupo Manyara Safari Lodge ya Manyara, Serengeti Heritage Luxury Camps, Ndutu Camps and Lodge ya Ngorongoro na Serengeti Kaskazini", 

"Tofauti yetu na makampuni mengine ni kubwa kwa sababu wateja wakija kwetu wanapata kila kitu ikiwemo malazi safi, chakula kizuri, kufurahia wanyama mbugani, timu yenye ubobezi katika masuala ya kuongoza Watalii wenye lugha nzuri, na hii imekuwa sababu muhimu ya sisi kupata wageni katika vipindi vyote kwa maana ya  High Season na Low Season)" amesema Mashauri. 

Hata hivyo ameongeza  kuwa, maonyesho ya Karibu Kili Fair msimu huu yamekuwa makubwa na kuleta tija. Matarajio ni kuona Watalii wakiongezeka maradufu zaidi ya ilivyokuwa hapo awali, na kuwakumbusha Watanzania kutembelea vivutio vilivyopo nchini kwa sababu gharama zake ni nafuu tofauti na wageni kutoka nje kwa asilimia 40 ya kiasi wanachotoa. 

Share To:

Post A Comment: