Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kutangaza jina rasmi la Daraja la Kigongo- Busisi la Jijini Mwanza wakati atakapokuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wake unaotarajiwa kufanyika Juni 19, 2025.

Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega amebainisha hayo leo Jumapili Juni 08, 2025 wakati wa mjadala wa MamaNiMjenzi, uliofanyika Jijini Mwanza kwenye daraja hilo na kuhusisha Wanahabari kutoka vyombo kadhaa vya habari, akisema awali daraja hilo liliitwa JP Magufuli katika siku zake za mwanzo wa utekelezaji wa daraja hilo kama sehemu ya heshima kwa Hayati Magufuli aliyekuwa na maono ya ujenzi wake, kabla ya baadae kuitwa Kigongo- Busisi ambavyo ni vijiji vya pande mbili za daraja hilo.

Katika hatua nyingine, Waziri Ulega amebainisha kuwa daraja hilo limegharimu takribani Shilingi Bilioni 716 ikijumuisha Kodi ya VAT, fedha ambazo zinatokana na mapato ya ndani, fedha ambazo zimekwishalipwa ziote kwa Mkandarasi aliyetekeleza ujenzi huo.

Waziri Ulega pia amezungumzia matumizi ya wakandarasi wa ndani katika utekelezaji wa miradi mikubwa nchini, akisema daraja hilo limejengwa na Mkandarasi wa nje kutokana na kuhitaji teknolojia kubwa katika ujenzi wake.

Share To:

Post A Comment: