Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kusimamia vyema utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyoachwa na Mtangulizi wake Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimuombea afya njema na ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka huu.

Majaliwa amesema hayo leo Mjini Mwanza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo- Busisi, akieleza kuwa maono ya Ujenzi wa daraja hilo yalikuwa ya Dkt. John Magufuli na Rais Samia amefanikisha kukamilishwa kwake, kando ya miradi mingine mingi iliyoachwa katika hatua za awali za utekelezaji wake nchini.

"Kwa bahati nzuri sana, Mwenyenzi Mungu hamuachi mtu mwenye dhamira njema na mwenye Mapenzi mema kwa watu wake. Wewe Mhe. Rais una mapenzi mema kwa nchi hii, wewe una mapenzi mema kwa Watanzania na maelekezo yako kwa sisi wasaidizi wako, tumeendelea kusimamia maelekezo yako." Amesema Majaliwa.

Akiitaja miradi mingine iliyoachwa katika hatua za awali, Waziri Mkuu Majaliwa amesema mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR, Unaendelea huku Kipande cha Dar Es salaam- Dodoma kikiwa kimekamilika, Bwawa la kuzalisha Umeme la Mwalimu Nyerere limekamilika, Meli mpya Ziwa Viktoria imekamilika pamoja na Madaraja ya juu (Flyover) za Ubungo na Tazara Jijini Dar Es salaam ambayo yote yamekamilika.

Majaliwa pia amempongeza Rais Samia kwa maendeleo makubwa kwenye sekta za huduma ya Kijamii ikiwemo huduma za Maji, Elimu, Afya, Kilimo na ujenzi wa barabara za Mijini na Vijijini, akibainisha kuwa kwasasa kila Mtanzania anashuhudia hatua kubwa za maendeleo zilizopigwa kwenye maeneo yao.

Share To:

Post A Comment: