Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumatano Juni 19, 2025 akiwa Jijini Mwanza, amezindua rasmi Daraja la J.P Magufuli (John Pombe Magufuli), zamani daraja la Kigongo- Busisi lenye urefu wa Kilomita 3.0 pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa Kilomita 1.6, likitarajiwa kufungua fursa zaidi za kiuchumi Kanda ya Ziwa pamoja na kukuza utengamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Daraja la JP Magufuli limetajwa kywa refu zaidi katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, huku likishika nafasi ya sita kwa bara la Afrika, daraja lilaoongoza likiwa ni la 6th October lililopo nchini Misri lenye urefu wa Kilomita 20.5, Third Mainland la Nigeria (KM 11.8), Suez Canal la Misri (KM 3.9), Kisiwa cha Msumbiji (KM 3.8) na daraja la Dona Ana la nchini Msumbiji lenye urefu wa KM 3.67.
Baada ya uzinduzi wa daraja hilo, Rais Samia anatarajiwa kuzungumza na wananchi, Juni 20, akitarajiwa kuzindua mradi wa Maji Butimba uliogharimu takribani Bilioni 71 na kutarajiwa kuhudumiwa wananchi 450,000 wa Jiji la Mwanza na Viunga vyake kwa kuzalisha lita Milioni 48 za maji kwa siku pamoja na kukagua na kuzindua miradi mingine mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wannachi wa Mwanza.
Post A Comment: