Wananchi wa Kijiji cha Mvuleni na vijiji vya jirani katika Kata ya Nyamato,Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani wamenufaika na Huduma bora ya afya baada ya Ujenzi wa Kituo kipya cha Afya cha Mvuleni kilichogharimu Shilingi Milioni 559.
Kituo hicho kinachotoa Huduma za Wagonjwa wa nje,Huduma za Maabara,Upasuaji na Huduma za Uzazi, kimepunguza umbali kwa Wananchi kufata Huduma katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga.
Akizungumza wakati alipotembelea Kituo hicho,Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Ndg. Zainab Khamis Shomari (MNEC) amewataka Wananchi wa Kata ya Nyamato kuiunga Mkono Serikali ya Dkt. Samia Suluhu katika Juhudi zake za kuwaletea Maendeleo Watanzania.
"Katika maeneo yote tuliyozunguka tumekuta Vituo vya Afya,Zahanati na Maji Safi na Salama,hii ndio kazi inayofanywa na Serikali ya awamu ya Sita inayoongwa na Rais Samia Suluhu Hassan,lengo ni kusogea huduma muhimu kwa Wananchi"
Post A Comment: