Na Magesa Magesa, Arusha
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),Mohamed Mchengerwa ameziagiza halimashauri zote za majiji,manispaa,Wilaya na Miji kuhakikisha kuwa zinawalipa madiwani stahiki zao kwa wakati.
Aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza kwa njia ya simu na madiwani wa Halimashauri ya Jiji la Arusha,wakati wa zoezi la ufungaji wa baraza la madiwani na kusema kuwa agizo hilo ni kwa nchini nzima.
“Kwanza niwapongeze kwa kusimamia halimashauri katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo mpaka leo mnapofika tamati ya kikindi chenu cha miaka mitano,nawaagiza wakurugenzi wawalipe stakiki zenu ikiwemo mafao haraka iwezekanavyo”alisisitiza Waziri huyo.
Kadhalika Mchengerwa alimaliza taharuki iliyokuwepo ya kuwataka madiwani kurudisha Vishikwambi walivyokuwa wam,ekabiziwa na halimashauri kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao,ambapo tayari walikwisha kutangaziwa kuvirudisha pindi tu wamalizapo muda wao,na kuagiza mamlaka husika kutokuvichua na badala yake wawaachie.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye ndiye alikuwa Mgeni Rasmi katika tukio hilo aliwapongeza madiwani wa halimashauri zote za mkoa wa Arusha kwa utendaji kazi wao katika kusimamia miradi mbalimbali ya kimaendeleo inayotekelezwa na halimashauri.
Kadhalika Makonda alionesha kukerwa kwake kwa kitendo cha Wenyeviti wa Mitaa,Vijiji na vitongoji kulipwa stahiki zao kupitia ofisi ya Afisa mtendaji wa Kata na kuagiza kuanzia sasa kila mwenyekiti alipwe kupitia akaunti yake.
“Si jambo jema eti Mwenyekiti wa Mtaa,Kijiji na Kitongoji mpaka aende kwa mtendaji ndo apate stahiki zake,Naagiza kuanzia sasa Wenyeviti wote walipwe stakiki zao moja kwa moja kupitia akaunti zao”alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Akivunja Baraza hilo la Madiwani wa Halimashauri ya jiji la Arusha,Mstahiki Myeya wa jiji hilo,Maximillian Iranqe aliwapongeza madiwani wote kwa kufanya kazi pamoja kwa na kwa ushirikiano katika kipindi chote walichokuwepo hapo,
Kazalika aliwapongeza wafanyakazi wote wa halmashauri wakiongozwa na mkurugenzi wa jiji katika usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuongeza kuwa hadi wao wanaondoka mapato ya Halimashauri yameongezeka kutoka Bilioni22 na kufikia bilioni 51
Post A Comment: