NA DENIS MLOWE IRINGA

MAELFU ya wananchi na wanachama wa CCM mkoa wa Iringa jana walivunja rekodi ya mapokezi ya kumkaribisha Asas, ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kupitia Mkoa wa Iringa (MNEC) baada ya kuchuguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Ccm Taifa.


Akizungumza wakati wa mapokezi hayo, Asas alitoa shukrani kwa wanachama wa CCM mkoani Iringa kwa kumpa heshima ya kuwa miongoni mwa waliomuwezesha kufikia uteuzi huo mkubwa katika Chama cha Mapinduzi.


Asas alisema kuwa bila nyinyi kunichagua kuwa MNEC, nisingekuwa chama hiki kikubwa kisingenichagua kuwa Mcc hivyo natoa shukrani kwa wanachama wote na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan na wajumbe wa NEC kuridhia niwe kwenye nafasi hiyo.


Alisema kuwa mara baada ya uteuzi huo amekuja na Ajenda mbili muhimu ambazo ya kwanza ni kuhakikisha chama kinashika dola ambapo ndio lengo la kila chama cha siasa nchi yoyote na hii ina maanisha atahakikisha Rais Samia anashinda kwa kishindo mkoani hapa na mikoa mingine ya Tanzania.


Kutokana na nia hiyo Salim Asas alisema atahakikisha ushindi huo kwa kwa kufanya ziara ziwe pori kwa pori, mtaa kwa mtaa, kuhakikisha Mama anapata kura za kutosha. Haiwezekani Mjumbe wa Kamati Kuu atoke Iringa halafu kura za mama ziwe za mashaka hivyo ushindi wa kishindo lazima.


Alisema kuwa ajenda ya pili ni Kuhudhuria vikao na kutenda haki kwa kila mmoja katika kuwajadili wagombea na wanachama na kuomba ushirikiano katika kufanya shughuli za chama kuanzia ngazi ya mkoa hadi taifa.


Salim Abri aliwakumbusha uxito wa kazi hiyo wanachama na kusema kuwa ingekuwa na uamuzi, nisingependa shughuli kama hii isifanyike kutokana na ukubwa wake kwani  nafasi ya kusherehekea, ni nafasi nzito yenye wajibu mkubwa kwa chama na taifa na kusisitiza ukikosea, unaharibu sura ya chama na aliyekupendekeza,


Aliongeza kuwa kutokana na nafasi hiyo ameanza kupitia Katiba ya CCM kipengele kwa kipengele, akisema nafasi hiyo aliyopewa inashtua mwili kwa jinsi inavyobeba majukumu mazito ya chama na nchi kwani ukisoma Katiba ya chama chetu na majukumu ya Kamati Kuu, mwili unasisimka hii si nafasi ya kupendelewa, ni nafasi ya kufanya kazi kwa moyo safi kwa ajili ya chama na aliwakumbusha wanachi na wanachama wa CcM kuwa yeye atabaki kuwa yule yule na hatobadilika kwa sababu ya cheo na kueema kuwa cheo ni dhamana tu

Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Daudi Yasin, alimpongeza Asas akisema Zawadi ya kipekee tutakayompa Dk Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha anapata mitano mingine kwa kura nyingi mkoani Iringa na kata zote na majimbo yote CCM wanashinda kwa kishindo.


Katika sherehe hizo za kumkaribisha Viongozi mbalimbali wa CCM na serikali  akiwemo Mstahiki Meya wa Manispaa, wabunge na mawaziri, madiwani, viongozi wa mashina, wasanii, bodaboda, bajaji, machinga na wazee wa kimila walihudhuria na baadhi yao kuzungumza pongezi mbalimbali na kumwelezea MCC Salim Abri moyo wake wa kujitoa kwenye jamii.

Wabunge wa mkoa wa Iringa  wakiongozwa na Mbunge wa Iringa mjini, Jesca Msambatavangu, viti maalum Rose Tweve, Mbunge wa Kalenga Jackson Kiswaga na mbunge wa Kilolo Justine Nyamoga walisema kwa Salim Asas, jina lake sasa limeunganishwa moja kwa moja na hatima ya ushindi wa chama kwa ngazi zote na kilichomfikisha Salim Asas hapo ni nidhamu na utendaji kazi wake na kumpongeza kwa kuwa Mcc.

Mbunge wa Viti Maalumu, Rose Tweve alisema kilichomfikisha Asas katika nafasi ya juu ya chama hicho ni nidhamu na utii kwa chama chake hivyo ni wakati sqhihi wa viongozi kujifunza  nidhamu na kujitoa ndani ya chama na wananchi kwa ujumla.


Mbunge wa Iringa Mjini, Jesca Msambatavangu alisema kwa utendaji kazi wa Salim Abri hakika anastahili hiyo nafasi ambayo ni kubwa ndani ya chama na kumpongeza kwa utendaji kazi wake iliotukuka ndani na nje ya chama.


Kabila la wahehe wakiongozwa Chifu Adam Abdul Sapi Mkwawa walimsimika kuwa chifu wa kabila hilo Salim Asas na kusema kuwa Salim amekuwa mtu muhimu ndani ya jamii ya Iringa kutokana mambo mbalimbali ya kimaendeleo aliyoyafanya.


Naye wakili wa kujitegemea mkazi wa jimbo la Kalenga ambaye naye amekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Kalenga, Sosten Mbedule alisema kuwa uteuzi wa Salim Asas kama umechelewa katika kuteuliwa kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya ndani na nje ya mkoa wa Iringa, ndani ya chama na nje ya chama. 

Alitumia nafasi hiyo kumpongeza kuwa Mcc na kutoa shukrani kubwa kwa Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumwona Salim kwani anastahili nafasi hiyo na muda sahihi katika kuelekea kwenye uchaguzi kutoka na ushawishi mkubwa alionao Mnec na Mcc Abri.

    

Share To:

Post A Comment: