Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro (RAS), Yusufu Nzowa, amesema amepokea barua inayoelekeza Madiwani wote, kurejesha vitendea kazi vyote, vikiwemo vishikwambi na chaja zake. 

Amesema hayo leo, Jumatano Juni 18,2025 alipokuwa akitoa hotuba ya kulivunja Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wlaya ya Siha, mkoani humo. Kwa mujibu wa Nzowa, maelekezo hayo kwa Madiwani, ni takwa la kisheria. 

Amesema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, ameelekeza hayo pamoja na mambo mengine katika waraka rasmi wa kuvunjwa mabaraza ya madiwani katika halmashauri zote nchini ifikapo Juni 20 mwaka huu.

 "Vifaa hivi vimenunuliwa na fedha za umma, ni jambo la kiungwana madiwani wote kuvirudisha kwa maendeleo ya Halmashauri kwa siku zijazo. ...Kwa sasa, Baraza linavunjwa, nikuagize Mkurugenzi na wataalamu, hakikisheni miradi iliyoachwa na Madiwani, misimamie na kuiendele na sio kuibadilisha na kuanza yakwenu, labda kama kuwe kuna ulazima huo,"amesema. 


Source : Nipashe

Share To:

Post A Comment: