Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameliambia Bunge la Tanzania leo Ijumaa Juni 27, 2025 kuwa Tanzania itapata Katiba Mpya ndani ya Miaka mitano ijayo ili kujibu Rai ya muda mrefu ya wadau wa siasa nchini Tanzania.

"Kwakuwa suala la Katiba ni pendekezo la muda mrefu la Tume ya maridhiano, kwa msingo huo mchakato wa Katiba mpya ni miongoni mwa ahadi ambazo zinaonekana katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya 2025/30, hivyo nikusema kwamba shughuli ya kuanza kupata Katiba mpya itatekelezwa katika kipindi kijacho cha miaka mitano." Amekaririwa Rais Samia.

Kauli hiyo ameitoa leo Bungeni Mjini Dodoma wakati wa Hotuba yake ya kuhitimisha shughuli za Bunge la 12 la Tanzania, akisisitiza dhamira yake ya kuwa na Taifa lenye maelewano na maridhiano ili kwenda kwenye dhima ya maendeleo bila ya kumuacha yeyote nyuma.

Rais Samia pia amebainisha mafanikio ya falsafa yake ya 4R iliyosisitiza kuhusu mageuzi, maridhiano, ustahimilivu na kujenga upya ambapo amebainisha kuwa wadau mbalimbali waliletwa pamoja na ufanya maamuzi na maboresho ya pamoja yaliyowezesha mabadiliko ya sheria na kurejeshwa kwa mikutano ya hadhara na shughuli za kisiasa nchini Tanzania.

Amebainisha kuwa miongoni mwa mabadiliko hayo ni pamoja na kutungwa kwa sheria mpya ya Tume huru ya Taifa ya uchaguzi, sheria ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani (2) ya mwaka 2024 pamoja na sheria ya Vyama vya siasa na sheria ya Gharama za uchaguzi.

Aidha Rais Samia pia amebainisha kuwa ruzuku za ya Bilioni 87.87 imetolewa kwa Vyama vya siasa vinavyostahili huku pia asasi za Kiraia zikiwa huru kufanya shughuli zao sambamba na kuimarika kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania.



Share To:
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post A Comment: