Kamati ya Siasa ya halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi mkoa wa Njombe imetoa maelekezo kwa kamati za siasa wilaya zote mkoani humo kuwachukulia hatua wanachama na viongozi wote wa chama hicho wanaoandika maneno yenye kukejeli na kutukana viongizi mitandaoni.
Akitoa taarifa ya kikao cha kawaida cha kamati ya Siasa kilichofanyika mkoani humo,katibu wa Siasa na Uenezi mkoa wa Njombe Josaya Luoga amesema kikao hicho kilichokuwa na lengo la kujadili mambo mbalimbali ya Chama lakini pia kimetoa maelekezo hayo ili kudhibiti sintofahamu zinazotengenezwa na kuharibu kazi za Chama.
"Kamati ya Siasa ya halmashauri kuu ya mkoa imetoa maelekezo kwa kamati za Siasa za wilaya na kamati za maadili kuhakikisha zinafanya kazi ya kuwaita watu wote wanaochapisha mitandaoni maneno yanayo ashiria kutengeneza sintofahamu kwenye makundi sogozi na kuwachukulia hatua"amesema Luoga
Amesema "Wale wote ambao wataonekana kweli wameandika na kuthibitika watachukuliwa hatua kali kuhakikisha chama kinakuwa tulivu kuelekea uchaguzi 2025 tuwapate viongozi ambao watakwenda kufanya kazi za wananchi kwa utulivu"
Luoga amewataka wanachama na viongozi wa Chama hicho kuchukua tahadhari na mandishi yanayochapishwa mitandaoni ambapo ametoa rai kwa wanachama kuandika maneno yanayolenga umoja na mshikamano wa Chama cha Mapinduzi.
Post A Comment: